Recho Ray akanusha kughushi noti ya shillingi elfu 50 Uganda

Recho Ray akanusha kughushi noti ya shillingi elfu 50 Uganda

Msanii Recho Ray amejitenga na picha inayosambaa mtandaoni ikimuonesha akiwa kwenye noti ya shilling elfu 50 ya Uganda ambapo alikuwa ameanika wazi maungo yake ya mwili. Recho Ray anasema picha hizo zilichapishwa na watu waliodukua akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Facebook. β€œHey, guys my account is restored now. It was hacked,” Aliandika Instagram. Lakini mashabiki zake wanahoji kuwa anajaribu kukwepa msala wa kufunguliwa kesi kwa madai ya kughushi nyaraka za serikali. Ikumbuke ni kosa la jinai kwa mtu yeyote kuchapisha noti au sarafu yoyote ya Benki Kuu nchini Uganda.

Read More
 RECHO RAY AKIRI USHIRIKINA KUSHEHENI KWENYE MUZIKI WA UGANDA

RECHO RAY AKIRI USHIRIKINA KUSHEHENI KWENYE MUZIKI WA UGANDA

Msanii Recho Ray amefunguka na kudai kwamba tasnia ya muziki nchini Uganda imesheheni ushirikina. Katika mahojiano yake hivi karibuni Recho amesema nguvu za giza ndio chanzo ya baadhi ya wasanii wakongwe nchini humo kusalia kwenye muziki kwa muda mrefu. Mrembo huyo amesema wasanii wengi wenye vipaji wamepotea kimuziki kutokana na baadhi ya wadau nchini Uganda kutumia hirisi kuua mafanikio yao. Recho Ray ambaye ulimwengu wa muziki ulimfahamu mwaka 2018 kupitia wimbo wake uitwao “Who is Who” amekuwa akisuasua kwenye muziki wake bila kuachia hitsong yeyote. Utakumbuka mrembo huyo sio msanii wa kwanza kudai kuwa kiwanda cha muziki nchini Uganda imetawala ushirikina, miezi kadhaa iliyopita msanii Nince Henry aliibuka na kuwatolea uvivu wasanii wote wanaoishi Makindye kwa tuhuma za kuwadhamini sana waganga wa kienyeji kwenye suala la kusafisha nyota yao ya muziki.

Read More