REMA NAMAKULA AFUNGUKA SABABU ZA KUTOANIKA NDOA YAKE MTANDAONI
Msanii Rema Namakula has ameonyesha kuchukizwa na waganda kwa kuwa roho na roho mbaya. Katika mahojiano yake hivi karibuni Rema amesema siku hizi huwa haposti tena mume wake kwenye mitandao ya kijamii akieleza kuwa waganda wengi hawamtakii mema. Hitmaker huyo wa ngoma ya Gutujja amesema aliacha kuanika maisha yake ya mahusiano baada ya mashabiki wake kudai kuwa uhusiano wake na mumewe utaishia kwa kilio tu. “When I discovered that Ugandans are evil-hearted, I stopped showing them what makes me happy. At first, I thought if you are happy, you should just feel free. Let it all out because it’s normal but I realized it is not okay with some people,” she explained. Katika hatua nyingine ameeleza kuwa anaendelea kushirikiana na Eddy Kenzo kutoa matunzo kwa binti yao ambaye walizaa pamoja. Rema namakula amesema hawana utofauti wowote na eddy kenzo kwenye masuala ya kutoa malezi kwa mtoto wao kama wengi wanavyodhani. Utakumbuka Rema namakula aliachana na eddy kenzo mwaka wa 2019 ambapo aliingia kwenye mahusiano mengine na Hamsa Ssebunya
Read More