Spice Diana Afichua Siri Nzito ya Uchawi Miongoni mwa Wasanii Uganda
Msanii maarufu wa Uganda, Spice Diana, ametikisa tasnia ya burudani kwa madai mazito ya kuwepo kwa uchawi miongoni mwa wanamuziki. Katika mahojiano a Galaxy TV, msanii huyo wa “Source Management” alieleza kuwa baadhi ya wasanii hutumia nguvu za giza kwa lengo la kudhoofisha na kuvuruga mafanikio ya wenzao. “Watu wanafanya kazi kwa bidii gizani kuhakikisha wanaharibu kazi za wenzao. Tuwe wakweli – haya mambo yapo,” alisema Spice Diana kwa msisitizo Licha ya kuwa na imani kwamba uchawi upo katika sekta ya muziki, Spice Diana anasema hajawahi kuathirika moja kwa moja na uchawi huo. Anaamini kuwa nguvu ya maombi kutoka kwa mashabiki wake na imani yake kwa Mungu ndiyo ngao yake. “Labda mtu alijaribu kuniroga lakini akashindwa. Mungu amenilinda kupitia maombi ya mashabiki wangu wengi,” alisema. Hata hivyo, msanii huyo aliongeza kuwa si kila changamoto inayompata msanii ina uhusiano na uchawi. Alisisitiza kuwa matatizo ya kawaida ya kibinadamu pia huwapata wasanii kama watu wengine. “Wakati mwingine tunapitia matatizo ya kawaida kama binadamu wengine, lakini tunadhani tumerogwa. Ndio maana sitaki kila tatizo ninalopitia niunganishe na uchawi,” alieleza. Kauli ya Spice Diana imezua mijadala mikali katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, huku baadhi wakimsifu kwa ujasiri wake wa kusema ukweli, na wengine wakihofia kuwa madai hayo yanaweza kuongeza hofu na chuki miongoni mwa wasanii. Hili si tukio la kwanza kwa madai ya aina hiyo kusikika. Wasanii wengine kama Zanie Brown na Grace Nakimera pia wamewahi kuelezea masaibu waliyopitia kutokana na kile walichodai kuwa ni hujuma za kishirikina kutoka kwa wenzao katika muziki.
Read More