Rotimi afunguka kwanini anataka kuwa na watoto wengi

Rotimi afunguka kwanini anataka kuwa na watoto wengi

Mwanamuziki mwenye asili ya Nigeria Rotimi amefichua sababu kwa nini anataka kuwa na watoto wengi. Akizungumza kwenye video iliyochapishwa kwenye ukurasa wake wa Instagram Juzi, Rotimi alikiri kwamba kuwa mtoto wa pekee katika familia yao kulimfanya kutaka kuwa na watoto wengi. “Kwa hiyo nataka mwanangu (Seven Adeoluwa Akinosho) awe na mtu ambaye anaweza kumtegemea, ambaye anamuangalia. Wanajua watakuwa pale kwa ajili yake. Binti yangu akiangalia upande wake wa kulia, anajua ana kaka mkubwa ambaye anapitia jambo lile lile katika umri huo huo.” alisema Rotimi na kuongeza kuwa hakutaka kusubiri muda mrefu sana kupata watoto. “Unajua sikutaka lile pengo la miaka sita, saba ambapo kimsingi ni watoto tu, kwa hiyo nilitaka wawe karibu sana kiumri na Vanessa alielewa na yeye alitaka jambo hilo hilo. Nilihisi kuwa na mwenza huyo.” alieleza Rotimi. Mapema mwezi huu wawili hao walitangaza kuwa wanataraji

Read More
 Msanii wa Bongofleva Vanessa Mdee na mchumba wake Rotimi mbioni kupata mtoto wa pili

Msanii wa Bongofleva Vanessa Mdee na mchumba wake Rotimi mbioni kupata mtoto wa pili

Msanii wa Bongofleva Vanessa Mdee na mchumba wake Rotimi baada ya kuweka wazi wanatarajia kupata mtoto wao wa pili pamoja, na ni mtoto wa Kike, hatimaye wameamua kuonyesha ujauzito wa kijacho hicho ulipofikia. Wote wameshare video hiyo kupitia kurasa zao za Instagram. Aidha, wawili hao wameamua kufanya hivyo pia wakipromote na smash hit ya Rotimi akishirikiana na Nektunez iitwayo “Make You Say”. Link kwenye bio ya Rotimi. Itakumbukwa, wawili hao mtoto wao wa kwanza ni wa Kiume aitwaye Seven, walibarikiwa kumpata Septemba mwaka 2021

Read More
 VANESSA MDEE MBIONI KUONGEZA MTOTO WA PILI NA ROTIMI

VANESSA MDEE MBIONI KUONGEZA MTOTO WA PILI NA ROTIMI

Msanii wa Bongofleva Vanessa Mdee ni kama amenogewa na watoto, baada ya kumpata mtoto wake wa kwanza (Seven Adeoluwa Akinosho) na Rotimi mwezi Septemba mwaka huu. Vee Money leo kupitia ukurasa wake wa Instagram,ametangaza matamanio yake ya kuongeza mtoto mwingine. Vanessa ameweka video ya Rotimi akimbebeleza mtoto wao huyo wa Kiume na kisha kuacha caption ambayo mwisho alimalizia kwa kusema “Baby number two loading” akimaanisha mtoto wa pili yupo njiani. Itakumbukwa kwenye moja ya mahojiano aliyowahi kufanya, Vee alinukuliwa akisema anatamani kuwa na watoto wawili.

Read More