Kocha wa Saudi Arabia akanusha taarifa za wachezaji wake kupewa Rolls Royce

Kocha wa Saudi Arabia akanusha taarifa za wachezaji wake kupewa Rolls Royce

Kocha wa timu ya Taifa ya Saudi Arabia Herve Renard amekanusha taarifa zilizosambaa kwenye mitandao zikisema kwamba wachezaji wote wa timu hiyo watazawadiwa magari aina ya Rolls Royce kufuatia ushindi wao mkubwa dhidi ya Argentina kwenye fainali za Kombe la Dunia nchini Qatar. Kwa mujibu wa The New York Post, Herve Renard amesema hakuna ukweli kwenye taarifa hiyo “Hakuna ukweli wowote kuhusu hili. Tuna Shirikisho imara pamoja na Wizara ya Michezo. Na huu sio muda wa kupata chochote. Muhimu zaidi kwetu ni kumaliza 1 au 2 kwenye kundi.” alisema Kocha Renard. Taarifa hizo za wachezaji kupewa zawadi ya gari aina ya Rolls-Royce na Prince Mohammed Salman, zimekanushwa pia na Mshambuliaji wa timu hiyo, Saleh al-Shehri.

Read More
 Saudia Arabia yaichapa Argentina kwenye michuano ya Kombe la Dunia

Saudia Arabia yaichapa Argentina kwenye michuano ya Kombe la Dunia

Mitanange ya Kombe la Dunia inaendelea kutimua vumbi huko Qatar, ni timu 32, sawa na mechi 64 zikitarajiwa kupigwa kwenye viwanja tofauti. Moja kati ya mchezo uliwashangaza wengi Duniani ni huu wa mchana, ni mtanange wa Timu ya Taifa ya Argentina dhidi ya Saudi Arabia ambapo Argentina imeanza kwa kupigwa katika mchezo wake wa kwanza katika kundi C. Argentina ambayo iliyotangulia kufunga bao la kwanza kupitia kwa nyota wao Lionel Messi, imepoteza mchezo huo kwa mabao 1-2 dhidi ya Saudi Arabia ambao kwenye mchezo huo, walikuwa ni kama “Underdog” lakini wamefanya maajabu yasiyotarajiwa na wengi.

Read More