Mitanange ya Kombe la Dunia inaendelea kutimua vumbi huko Qatar, ni timu 32, sawa na mechi 64 zikitarajiwa kupigwa kwenye viwanja tofauti.
Moja kati ya mchezo uliwashangaza wengi Duniani ni huu wa mchana, ni mtanange wa Timu ya Taifa ya Argentina dhidi ya Saudi Arabia ambapo Argentina imeanza kwa kupigwa katika mchezo wake wa kwanza katika kundi C.
Argentina ambayo iliyotangulia kufunga bao la kwanza kupitia kwa nyota wao Lionel Messi, imepoteza mchezo huo kwa mabao 1-2 dhidi ya Saudi Arabia ambao kwenye mchezo huo, walikuwa ni kama “Underdog” lakini wamefanya maajabu yasiyotarajiwa na wengi.