Spice Diana Afichua Mbinu Aliyotumia Kukwepa Rushwa ya Ngono

Spice Diana Afichua Mbinu Aliyotumia Kukwepa Rushwa ya Ngono

Msanii nyota wa muziki kutoka Uganda, Spice Diana, amefunguka kuhusu changamoto alizokumbana nazo mwanzoni mwa safari yake ya muziki, akieleza namna alivyokwepa wanaume waliotaka kutumia nafasi zao kumshawishi kwa rushwa ya ngono. Akizungumza katika mahojiano na kituo kimoja cha televisheni nchini Uganda, Spice Diana amesema katika kipindi ambacho alikuwa bado anatafuta mafanikio kwenye tasnia ya muziki, alikutana na watu kadhaa waliomfuata wakiahidi kumsaidia kukuza kazi yake ya muziki kwa masharti ya mahusiano ya kimapenzi. Msanii huyo ambaye amedumu katika tasnia ya burudani kwa takribani miaka 15, amesema wengi wa watu hao walijitambulisha kama mameneja wa muziki au mapromota waliodai kuwa na uwezo wa kumfungulia milango ya mafanikio. Hata hivyo, Spice Diana amesema alitumia mbinu ya kipekee ili kujilinda dhidi ya shinikizo hilo. Amesema aliwageuza wanaume wote waliomfuata kwa nia hizo kuwa marafiki wa kawaida badala ya kukubali mahusiano ya kimapenzi waliyojaribu kumlazimisha. Kwa mujibu wa msanii huyo, mbinu hiyo haikuwa rahisi kwa baadhi yao, lakini ilimsaidia kuendelea kujenga kazi yake ya muziki bila kukubali masharti aliyoyaona si sahihi. Spice Diana pia ameonya kuwa hali kama hiyo mara nyingi huwakumba wasanii chipukizi wa kike ambao bado wanatafuta nafasi ya kung’ara kwenye tasnia ya muziki, huku baadhi ya watu wakitumia udhaifu huo kujaribu kuwashawishi kwa ahadi za mafanikio.

Read More
 Spice Diana Ahamasisha Wanawake Kujitegemea na Kufanya Kazi kwa Bidii

Spice Diana Ahamasisha Wanawake Kujitegemea na Kufanya Kazi kwa Bidii

Msanii nyota kutoka Uganda Spice Diana amewahimiza wanawake kufanya kazi kwa bidii na kujitegemea kifedha badala ya kutegemea wanaume ili kuendesha maisha yao. Msanii huyo ambaye amedumu kwenye tasnia ya muziki kwa karibu miaka kumi na tano amesema kuwa wanawake wana nafasi kubwa ya kujenga maisha yao na kuchangia maendeleo ya jamii ikiwa watachagua kujituma na kutumia fursa zilizopo. Akizungumza kuhusu umuhimu wa kujitegemea, Spice Diana amewashauri wanawake kuacha tabia ya kutegemea wanaume na badala yake wajitahidi kujenga mafanikio yao wenyewe. Msanii huyo ameongeza kuwa wanawake wataendelea kukumbana na changamoto na kudharauliwa iwapo hawatachukua hatua za kudhibiti maisha yao na kutumia fursa zilizopo katika kizazi cha sasa.

Read More
 Spice Diana Adai Hutumia Milioni 2 za Uganda kwa Siku

Spice Diana Adai Hutumia Milioni 2 za Uganda kwa Siku

Msanii nyota kutoka Uganda, Spice Diana, amefunguka kuhusu kiwango cha pesa anachotumia kwenye mahitaji yake kila siku. Akizungumza katika mahojiano na kituo kimoja cha runinga nchini humo, Spice Diana amesema kuwa hutumia takribani shilingi milioni 2 za Uganda kwa siku, hasa anapokuwa na shoo. Amesema hata anapokuwa nyumbani bila kufanya maonesho wala kulipa bili kubwa, bado matumizi yake hufikia karibu milioni 1.5 kwa siku. Kwa mujibu wa mrembo huyo, matumizi hayo yanajumuisha kujitunza binafsi, gharama za usafiri, chakula, maandalizi ya kazi (logistics) pamoja na mahitaji ya jumla ya maisha. Hata hivyo, Spice Diana anaamini kuwa mafanikio yana gharama, na kwa msanii wa kiwango chake, kuwekeza kwenye mwonekano na uendeshaji wa kazi ni sehemu ya safari ya mafanikio. Kauli yake imeibua mjadala mpana mitandaoni, ambapo baadhi ya mashabiki wanamsifia kwa uwazi na kujituma kuwekeza kwenye chapa (brand) yake, huku wengine wakiona kiwango hicho cha matumizi ni kikubwa kupita kiasi.

Read More
 Spice Diana Ashangazwa na Ukuaji wa Wafuasi Wake Mitandaoni

Spice Diana Ashangazwa na Ukuaji wa Wafuasi Wake Mitandaoni

Msanii nyota wa muziki kutoka Uganda, Spice Diana, ameonesha mshangao mkubwa baada ya kushuhudia ongezeko kubwa la wafuasi wake katika mitandao mbalimbali ya kijamii tangu kuanza kwa mwaka huu wa 2026. Kupitia Instastory yake, Spice Diana amesema awali alidhani kuwa umaarufu mkubwa mtandaoni huja zaidi na drama, lakini kwa sasa yupo katika kipindi cha amani na bado mafanikio yanaongezeka. Msanii huyo amefichua kuwa Snapchat views zake zimekuwa za kushangaza, huku TikTok akifikisha zaidi ya wafuasi milioni 2.3. Aidha, ndani ya siku 30 zilizopita pekee, akaunti yake ya Instagram imekusanya zaidi ya views milioni 4. Ingawa amekiri kuwa idadi hizo zimepungua kidogo katika siku chache zilizopita, amesema bado hali ni nzuri. Sambamba na mafanikio hayo, Spice Diana pia ametangaza kuwa dili mpya ya endorsement iko njiani, ishara kuwa ushawishi wake wa kidijitali unaendelea kuimarika. Kauli yake imekuja mara baada ya kufichua mwaka jana kuwa hatofanya tamasha lolote la muziki mwaka huu, akieleza kuwa ameamua kuelekeza nguvu zake katika kuwekeza zaidi kwenye majukwaa ya kidijitali.

Read More
 Spice Diana Aitaka Serikali Kufungua Facebook na Kudhibiti TikTok

Spice Diana Aitaka Serikali Kufungua Facebook na Kudhibiti TikTok

Msanii wa muziki kutoka Uganda, Spice Diana, ametoa wito kwa serikali ya Uganda kufungua kikamilifu mtandao wa Facebook, akisema kufungwa kwake kumeathiri biashara na wabunifu wa maudhui nchini humo. Akizungumza kwenye mahojiano hivi karibuni, Spice Diana amesema Facebook ni jukwaa muhimu kwa wajasiriamali na wasanii, lakini kufungiwa kwake kumepelekea watumiaji wengi kulazimika kutumia VPN, hali ambayo imezuia ukuaji wa biashara za kidigitali. Hata hivyo, msanii huyo amepongeza mchango wa TikTok katika kutoa fursa za kipato kwa vijana na wasanii, lakini akaomba kuwepo kwa miongozo madhubuti ya kudhibiti matumizi yake. Amesema kukosekana kwa kanuni kumesababisha baadhi ya watumiaji kutumia jukwaa hilo vibaya kwa kudhalilisha na kushambulia wengine. Spice Diana amesema licha ya ugumu wa kudhibiti mitandao ya kijamii, kuwepo kwa kanuni za busara kunaweza kuifanya TikTok kuwa salama na yenye manufaa kwa watumiaji wote, bila kuathiri ubunifu.

Read More
 Spice Diana Akataa Kuweka Wazi Uhusiano Wake wa Kimapenzi

Spice Diana Akataa Kuweka Wazi Uhusiano Wake wa Kimapenzi

Msanii nyota wa Uganda, Spice Diana, ameweka wazi kuwa yupo kwenye uhusiano wa kimapenzi lakini ameamua kuficha kwa sasa hadi pale atakapokuwa tayari kuuthibitisha rasmi mbele ya umma. Akizungumza kwenye mahojiano na kituo kimoja cha runinga nchini Uganda, Spice Diana amesema kuwa anafurahia maisha yake ya mapenzi kwa utulivu mkubwa, mbali na macho ya umma. Amebainisha kuwa ni marafiki wachache wa karibu pekee wanaofahamu undani wa uhusiano huo. Msanii huyo ameeleza kuwa ataamua kumtambulisha mpenzi wake hadharani pale tu atakapokuwa tayari kuchukua hatua kubwa zaidi maishani, ikiwemo kuthibitisha rasmi mipango ya ndoa. Amesema hapendi shinikizo la umma linapokuja suala la mapenzi, jambo linalomfanya awe makini zaidi kabla ya kutoa taarifa kwa mashabiki. Kauli hiyo ya Spice Diana inakuja wiki kadhaa baada ya tetesi kuzagaa mitandaoni zikidai kuwa msanii huyo alivishwa pete ya uchumba kwa siri akiwa nchini Uingereza. Hata hivyo, msanii huyo hakuthibitisha wala kukanusha moja kwa moja taarifa hizo, akisisitiza kuwa mambo ya mapenzi yanahitaji muda na faragha.

Read More
 Spice Diana Avishwa Pete ya Uchumba Nchini Uingereza

Spice Diana Avishwa Pete ya Uchumba Nchini Uingereza

Msanii nyota wa muziki kutoka Uganda, Spice Diana, ameripotiwa kuvishwa pete ya uchumba kwa siri nchini Uingereza. Taarifa hizo zimechochewa zaidi na mfululizo wa picha na video zilizosambaa mitandaoni zikionyesha mrembo huyo akiwa na pete mpya linaloonekana kama la uchumba. Katika picha hizo, Spice Diana anaonekana mwenye furaha kubwa huku akiwa kwenye mazingira yanayodaiwa kuwa ya sherehe ya faragha. Hata hivyo, hadi sasa haijabainika ni nani hasa aliyemvisha pete, jambo ambalo limeibua maswali na kuongeza uvumi mtandaoni. Kwa muda mrefu, Spice Diana amekuwa akihusishwa kimapenzi na aliyekuwa meneja wake, Roger Lubega, ingawa hakuna uthibitisho wowote uliowahi kutolewa kuhusu uhusiano huo.

Read More
 Spice Diana Ajitolea Kulipa deni la Promota Aliyetupwa Jela

Spice Diana Ajitolea Kulipa deni la Promota Aliyetupwa Jela

Mwanamuziki kutoka Uganda, Spice Diana, ameonyesha moyo wa huruma baada ya kuahidi kumsaidia promota wa matamasha Biggie Events, aliyetupwa gerezani Luzira Prison kwa kushindwa kulipa deni la takriban Ugx milioni 70, sawa na takriban KSh milioni 2.5. Kupitia mitandao ya kijamii, Spice Diana ameeleza kuguswa na hali ya promota huyo ambaye amekuwa akihangaika kurejesha mkopo aliouchukua kwa ajili ya kuandaa tamasha lililoshindwa kufanikiwa kibiashara. Msanii huyo amesema yuko tayari kuchangia kiasi cha fedha ili kumsaidia Biggie kutoka gerezani, akiwataka pia wasanii na wadau wengine wa muziki nchini Uganda kuungana naye katika juhudi za kumsaidia promota huyo kurejea uraiani. Biggie Events anafahamika kwa kuandaa matamasha kadhaa ya muziki nchini Uganda, yakiwemo yale yaliyowahi kumhusisha Spice Diana na wasanii wengine wakubwa.

Read More
 Spice Diana Akanusha Taarifa za Kushambuliwa Kuwa Kiki

Spice Diana Akanusha Taarifa za Kushambuliwa Kuwa Kiki

Mwanamuziki kutoka Uganda Spice Diana, amekanusha taarifa zinazosambaa mitandaoni zikidai kuwa tukio la kushambuliwa na wahuni waliokuwa wameabiri boda boda lilikuwa kiki au tukio lililopangwa kwa ajili ya kujitangaza. Katika taarifa, Spice Diana amesema uvumi kwamba tukio hilo lilipangwa kwa nia ya kujitangaza hauna msingi wowote, akifafanua kuwa wahuni walifuatilia gari lake kwa muda kabla ya kulishambulia. Mrembo huyo amesema uvamizi huo ulisababisha uharibifu mkubwa kwenye vioo vya nyuma na mlango wa nyuma wa gari. Hata hivyo, Spice Diana amebainisha kuwa yeye pamoja na marafiki zake waliokuwa ndani ya gari walinusurika bila majeraha. Spice Diana, ametoa shukrani kwa mashabiki wake kwa kumjali na kufuatilia hali yake, lakini akatoa wito kwa umma kutoamini wala kusambaza uvumi au taarifa za uongo kuhusu tukio hilo, akisisitiza kuwa taarifa rasmi zitatolewa kupitia akaunti zake zilizothibitishwa pekee. Tukio la Spice Diana kushambuliwa na wahuni liliripotiwa kutokea usiku wa Oktoba 17, wakati msanii huyo alipokuwa akirejea nyumbani eneo la Makindye baada ya sherehe za kabla ya siku yake ya kuzaliwa Akiwa njiani kupitia barabara ya Munyonyo, watu wasiojulikana waliokuwa kwenye boda boda walirusha mawe kwenye gari lake, na kusababisha vioo vya nyuma kuvunjika.

Read More
 Spice Diana Aeleza Sababu za Kukataa Kubadili Maumbile kwa Upasuaji

Spice Diana Aeleza Sababu za Kukataa Kubadili Maumbile kwa Upasuaji

Staa wa muziki kutoka Uganda, Spice Diana, ameweka wazi msimamo wake kuhusu wimbi la wasanii na wanawake wengi kugeukia upasuaji wa urembo au butt lift ili kubadilisha maumbile yao. Msanii huyo ambaye anafanya poa na single yake iitwayo “Award” amesema kuwa sababu kubwa inayomzuia ni hofu ya maumivu, akieleza kwamba hataki kitu chochote kinachoweza kuumiza mwili wake. Licha ya msimamo wake binafsi, mrembo huyo amesisitiza kuwa kila mtu ana uhuru wa kufanya maamuzi kuhusu mwili wake. Anaamini kuwa dunia ya sasa inaruhusu watu kuamua wanachotaka kufanya, iwe ni upasuaji, butt lift au mabadiliko mengine ya kimaumbile, na kwamba haifai mtu yeyote kulaumiwa au kukosolewa kwa uamuzi huo. Kauli ya Spice Diana inakuja wakati mjadala kuhusu upasuaji wa urembo unaendelea kushika kasi barani Afrika, huku baadhi wakiona ni njia ya kujiamini na wengine wakihofia madhara ya kiafya pamoja na viwango visivyo halisi vya urembo.

Read More
 Spice Diana Amshambulia Sheebah, Adai Analipa Wanablogu Kumchafua

Spice Diana Amshambulia Sheebah, Adai Analipa Wanablogu Kumchafua

Msanii nyota wa muziki nchini Uganda, Spice Diana, ameendeleza mashambulizi ya maneno dhidi ya msanii mwenzake Sheebah Karungi, akimtuhumu kuwalipa wanablogu na baadhi ya watu kutoka kwenye timu yake ili kusambaza taarifa za kumchafua mtandaoni. Akizungumza katika mahojiano na kituo cha runinga nchini Uganda, Spice Diana alisema kuwa Sheebah mara nyingi hujikita kumzungumzia kila anapopata nafasi, jambo ambalo kwa upande wake anadai halimsumbui. Spice Diana amesema kuwa hatua ya kum-unfollow Sheebah kwenye Instagram ilitokana na kile alichokiona kama tabia za kimaslahi binafsi na zisizo za ukweli. Alieleza kuwa badala ya kushughulikia masuala yao binafsi kwa njia ya moja kwa moja, Sheebah alichagua kuchapisha ujumbe kwenye mitandao ya kijamii, hali iliyomfanya apoteze imani naye. Kwa upande wake, Sheebah Karungi, kupitia mkutano na wanahabari uliofanyika wiki iliyopita, alikanusha madai ya kumshambulia Spice Diana au kulipa wanablogu waandike habari mbaya kumhusu, akieleza kuwa hana sababu yoyote ya kufanya hivyo. Mvutano kati ya wasanii hawa wawili umeendelea kushika kasi kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, huku mashabiki wakifuatilia kwa karibu maendeleo ya mzozo huo

Read More
 Jowy Landa Apinga Kauli ya Spice Diana Kuhusu Mafanikio Bila Kuwa na Hit songs

Jowy Landa Apinga Kauli ya Spice Diana Kuhusu Mafanikio Bila Kuwa na Hit songs

Mwanamuziki chipukizi kutoka Uganda, Jowy Landa, amejitokeza hadharani kupinga kauli ya Spice Diana kwamba mtu anaweza kufanikiwa katika muziki bila kuwa na nyimbo kali (hit songs). Kupitia mahojiano aliyofanya hivi karibuni na kituo cha redio, Jowy Landa alisema kuwa mafanikio ya kweli katika muziki hayawezi kupimwa kwa umaarufu wa mtu mtandaoni au mwonekano wa kisanaa pekee, bali kwa uwezo wa kutoa kazi zinazogusa mashabiki na kudumu kwenye chati. “Ni vigumu kusema umefanikiwa kama hauna hata wimbo mmoja ambao watu wanaweza kuuita hit. Mafanikio katika muziki yanatokana na impact unayoacha kwa wasikilizaji. Nyimbo kali huonyesha ubunifu na uwezo halisi wa msanii,” alisema Jowy. Kauli hiyo imeonekana kumlenga moja kwa moja Spice Diana, ambaye hivi majuzi alijinasibu kwamba amefanikiwa katika tasnia ya muziki licha ya kutoachia nyimbo nyingi zilizotamba. Mashabiki kwenye mitandao ya kijamii wamegawanyika, baadhi wakimuunga mkono Jowy kwa kusema kuwa muziki mzuri ndio unaojenga jina la msanii, huku wengine wakimtetea Spice Diana wakidai kuwa mafanikio ni pana zaidi na si lazima yaambatane na hit songs pekee.

Read More