SPICE DIANA AKANUSHA KUTOALIKA WASANII KWENYE UZINDUZI WA STARGAL EP

SPICE DIANA AKANUSHA KUTOALIKA WASANII KWENYE UZINDUZI WA STARGAL EP

Msanii wa Source Management, Spice Diana amepuzilia mbali uvumi unasambaa mtandaoni kwamba hakuwaalika baadhi ya wasanii kwenye uzinduzi wa EP yake mpya Star Gal. Katika mahojiano yake hivi karibuni amesema madai hayo hayana ukweli wowote kwa kuwa alituma mwaaliko kwa kila msanii kupitia uongozi wake. Mkali huyo wa ngoma ya “Tujooge” amesema hana ugomvi wowote na msanii yeyote nchini uganda na kama kuna msanii hakupokea barua ya mwaaliko, uongozi wake ndio wakulaumiwa kwa kutomfikishia ujumbe. Kauli ya Spice diana imekuja mara baada ya wasanii Gravity Omutujju na Lydia Jazmine kudai kuwa hawakupata mwaaliko wa kuhudhuria uzinduzi wa EP mpya ya Spice Diana

Read More
 ROGER LUBEGA AMJIBU GRAVITY OMUTUJJU, ADAI ANATUMIA JINA LA SPICE DIANA KUTAFUTA KIKI

ROGER LUBEGA AMJIBU GRAVITY OMUTUJJU, ADAI ANATUMIA JINA LA SPICE DIANA KUTAFUTA KIKI

Meneja wa Spice Diana, Roger Lubega amemjibu Gravity Omutujju kuonekana kumshambulia katika siku za hivi karibuni kwa kudai kwamba ni mnafiki na hajawahi watakiwa wasanii wengine mema kwenye muziki wao. Katika mahojiano yake Roger Lubega amesema hana ugomvi wowote na Omutujju huku akidai kuwa rapa huyo anatumia jina la msanii wake Spice Diana kutengeneza matukio ya kuzungumziwa mtandaoni kama njia ya kuitangaza tamasha lake litakalofanyika Cricket Oval Lugogo, Oktoba mosi mwaka huu. Kwa upande rapa Gravity Omutujju amepuzilia mbali madai ya lubega kwa kusema kwamba mambo yote aliyozungumza juu meneja huyo ni ya kweli huku akisema kwamba hawezi kutumia jina lake kutafuta kiki kwa kuwa yeye ni msanii mkubwa. Hata hivyo amesema amefanya matamasha makubwa ambayo yamepata mapokezi mazuri kutoka kwa mashabiki bila kutumia kiki huku akitishia kusitisha tamasha lake iwapo watu wataendelea kudai kwamba anatengeza matukio kwa ajili ya kutangaza tamasha hilo. Utakumbuka mwaka wa 2019 Gravity Omutujju aliwadanganya mashabiki zake kuwa alipigwa risasi tumboni lakini ilikuja ikabainika alitumia njia hiyo kwa ajili ya kutangaza show yake aliyoifanya katika ukumbi wa Cricket Oval Lugogo, nchini Uganda.

Read More
 SPICE DIANA AMJIBU GRAVITY OMUTUJJU KITAALAM

SPICE DIANA AMJIBU GRAVITY OMUTUJJU KITAALAM

Staa wa muziki kutoka nchini Uganda Spice Diana amemjibu rapa Gravity Omutujju kisomi baada ya rapa huyo kumshambulia kwa kudai kwamba ni mnafiki. Katika mahojiano yake Spice Diana amesema hana muda wa kupishana na Gravity Omutuju kwa kuwa ameelekeza nguvu zake zote kutangaza muziki wake ili uwafikie watu wengi duniani. Mwishoni mwa juma lilopita Gravity Omutujju alimshambulia Spice diana na meneja wake akidai kwamba wawili hao wana roho mbaya kwani hawajawahi watakia wasanii wengine mema. Gravity Omutujju alitoa kauli hiyo  baada ya spice diana kuwaalika wasanii wengi kwenye hafla ya uzinduzi wa EP yake mpya iitwayo Star Gal.

Read More
 SPICE DIANA AACHIA RASMI EP YAKE MPYA

SPICE DIANA AACHIA RASMI EP YAKE MPYA

Staa wa muziki kutoka nchini Spice Diana Uganda ameachia rasmi EP yake mpya iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki zake. EP hiyo inakwenda kwa jina la Star Gal ina jumla ya nyimbo 4 za moto ikiwa na kolabo mbili  kutoka kwa wakali kama Jose Chameleone, John Blaq na Daddy Andre. Star Gal ambayo kwa sasa inapatikana kwenye majukwaa yote ya ku-stream muziki duniani  ina ngoma kama Boss,Bwotyo,Sankalebwa na Toli Weka. Hii ni EP ya kwanza kwa mtu mzima Spice Diana tangu aanze safari yake ya muziki  na mwaka wa 2015.

Read More
 SPICE DIANA KUACHIA EP YAKE MPYA WIKI IJAYO

SPICE DIANA KUACHIA EP YAKE MPYA WIKI IJAYO

Staa wa muziki kutoka Uganda Spice Diana ameweka wazi tarehe ambayo EP yake mpya ya Star Gal itaingia sokoni. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Spice Diana amethibitisha kwamba Ep yake itaingia sokoni Mei 26 mwaka huu baada ya kukamilka kwa hafla ya usikilizaji wa Stargal EP ambayo pia itafanyika siku hiyo. Licha kuweka wazi tarehe ambayo ataachia EP yake Spice diana hajatuambia idadi ya ngoma pamoja na wasanii aliowashirikisha kwenye Stargal EP ila ni jambo la kusubiriwa. Stargal EP inaenda kuwa kazi ya kwanza kwa mtu mzima Spice Diana tangu aanze safari yake ya muziki miaka saba iliyopita.

Read More
 SPICE DIANA ADOKEZA UJIO WA EP YAKE MPYA

SPICE DIANA ADOKEZA UJIO WA EP YAKE MPYA

Nyota wa muziki kutoka Uganda Spice Diana ametangaza kuja na Extended Playlist ‘EP’ yake aliyoipa jina la ‘Stargal. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Spice Diana amewataka mashabiki wake kukaa mkao wa kula kuipokea EP yake hiyo ambayo kwa mujibu wake itaingia sokoni hivi karibuni. Pamoja na kutangaza ujio wa ep hajaweka wazi idadi nyimbo na wasanii aliowashirikisha kwenye EP yake ya Stargal Hii Inaenda kuwa EP ya kwanza kwa mtu mzima Spice Diana tangu aanze safari yake ya muziki miaka saba iliyopita

Read More
 SPICE DIANA AMSHAURI SHEEBAH KARUNGI KUWAAJIRI WALINZI

SPICE DIANA AMSHAURI SHEEBAH KARUNGI KUWAAJIRI WALINZI

Nyota wa muziki nchini Uganda Spice diana ameonekana kukerwa na kitendo cha msanii mwenzake Sheebah karungi kudhalalishwa kingono wiki iliyopita kwenye moja ya performance yake Katika mahojiano yake ya hivi karibuni Spice diana amelaani vikali kitendo cha msanii huyo kuvunjia heshima akiwa kwenye shughuli zake za kimuziki huku akitoa changomoto kwa Sheebah Karungi kuawaajiri walinzi watakaompa usalama kwenye shows zake. Hata hivyo Sheebah hajaweka wazi mwanamume aliyemdhalalisha kijinsia ila walimwengu kwenye mitandao ya kijamii wamehoji kuwa huenda ni professa. Gilbert Bukenya. ndiye aliyehusika. Utakumbuka mwaka 2020 aliwajiri walinzi kwa ajili ya kumpa usalama lakini watu walimkejeli kwa kusema kwamba ana walinzi wengi kuliko ngoma zake kali.

Read More
 SPICE DIANA ATOA WITO KWA WAANDAAJI WA TUZO UGANDA KUWAPA WASANII PESA

SPICE DIANA ATOA WITO KWA WAANDAAJI WA TUZO UGANDA KUWAPA WASANII PESA

Msanii nyota nchini Uganda Spice Diana amewataka waandaji wa tuzo nchini humo kuanza kuwapa wasanii pesa badala ya tuzo pekee. Akizungumza alipopokea tuzo ya msanii bora wa mwaka kutoka kwa kampuni ya MTN Uganda Spice diana amesema pesa inawafanya wasanii wajihisi vizuri zaidi ikizingatiwa wengi wao wamewekeza pesa nyingi kwenye kazi zao za muziki. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Mbikka” ametoa changamoto kwa waandaji wengine wa tuzo kufuata nyayo za MTN za kutambua juhudi za wasanii kwa kuwapa pesa pamoja na tuzo mtawalia. Kauli ya Spice diana imekuja mara baada ya kutunikiwa shillingi millioni 3 za Uganda kusindikiza tuzo ya msanii bora wa mwaka aliyopewa na kampuni MTM kupitia Callers Tune Awards. Utakumbuka kampuni ya mawasiliano ya MTN Uganda wikiendi hii iliyopita iliwazawadi tuzo  wasanii wote ambao nyimbo zao zilipakuliwa zaidi kama caller tunes kwa mwaka wa 2021.

Read More
 TINAH FIERCE APONDA UVAAJI WA SPICE DIANA,ASEMA HAJUI KUPENDEZA.

TINAH FIERCE APONDA UVAAJI WA SPICE DIANA,ASEMA HAJUI KUPENDEZA.

Malkia wa umbea nchini Uganda Tinah Fierce amefunguka na kusema msanii Spice Diana hajui kabisa kupendeza kwani mara nyingi hata nguo anazovaa ni kama zimetundikwa tu mwilini mwake. Tinah Fierce anasema wapo watu wengine wana pesa nyingi nchini Uganda  lakini suala la kuvaa kwao ni zero na kumtolea mfano Spice Diana kuwa ni moja ya watu ambao hajui kuvaa na hata nguo akivaa zinakuwa hazimkai vizuri mwilini Kupitia kipindi chake cha Random Thoughts ambacho kinaruka kupitia mtandao wa Youtube Tinah amemsuta vikali Spice Diana kwa  hatua ya kuvaa nguo za bei nafuu kutoka Uchina, na bila aibu ku-share picha zake akiwa amevali nguo hizo kwenye mitandao ya kijamii. Malkia huyo wa umbea ameenda mbali zaidi na kusema kwamba Spice Diana hapaswi kulalamika juu ya Tuzo za Janzi ikizingatiwa kuwa huwa hazungumzi kuhusu mambo mengine ambayo yanawaathiri watu wa kawaida. “Lala tu na uendelee kuvaa nguo zako za bandia na bei rahisi,” Tinah alisema. Ikumbukwe Tinah Fierce alifutwa kazi Urban TV kutokana na tabia yake ya kuwashambulizi watu maarufu nchini Uganda lakini sasa hivi chaneli yake ya YouTube  inampa uhuru wa kuzungumza chochote

Read More
 SPICE DIANA AKANUSHA BIFU LAKE NA MSANII MWENZAKE AZAWI

SPICE DIANA AKANUSHA BIFU LAKE NA MSANII MWENZAKE AZAWI

Nyota wa muziki kutoka nchini Uganda Spice Diana kwa mara ya kwanza amefunguka kuhusu suala la kuwa kwenye ugomvi na msanii mwenzake Azawi ambaye juzi kati ameshinda tuzo ya Janzi awards mwaka wa 2021. Hitmaker huyo wa “Upendo” amesema hana ugomvi na Azawi ambaye alishinda tuzo ya msanii bora wa kike kwenye tuzo za  Janzi Awards ila alikuwa anawakosoa waandaji wa tuzo hizo ambao walikuwa wanawatumia vibaya wasanii kwa maslahi yao binafsi. Spice Diana amesema ana furahia ushindi wa Azawi kwenye tuzo hizo kwani ni moja kati ya wadada ambao wameonyesha uwezo wa kipekee kwenye kazi zake za muziki. Ikumbukwe Spice Diana hakushinda tuzo hata moja kwenye tuzo za Janzi Awards licha ya kuwa na muendelezo mzuri wa kuachia kazi zake za muziki, jambo lilotafsiriwab na wajuzi wa mambo kuwa mrembo huyo ana machungu ya kutoshinda tuzo

Read More
 SPICE DIANA AZIPONDA TUZO ZA JANZI AWARDS 2021 KISA UPENDELEO

SPICE DIANA AZIPONDA TUZO ZA JANZI AWARDS 2021 KISA UPENDELEO

Mkali wa muziki kutoka Spice Diana ni muhanga wa tuzo mpya za Janzi Awards, ameibuka na kuwatupia lawama kwamba ni wala rushwa. Licha ya kuachia ngoma kali mwaka huu mrembo huyo alishindwa kuibuka na tuzo ya msanii bora wa mwaka kwenye tuzo za Janzi Awards 2021 ambazo zilifanya kwa mara ya kwanza katika Bustani ya Kololo Independence nchini Uganda. Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Spice Diana amewashutumu waandaji wa tuzo za Janzi kwa kashfa za rushwa na kuomba uwazi katika uteuzi. Hitmaker huyo wa “Upendo” amesema ameshindwa ni njia ipi waandaji wa tuzo za Janzi walitumia kumpata msanii aliyeshinda kipengele cha msanii bora wa mwaka. Spice Diana alikuwa akichuana na wasanii wengine wa kike kama Azawi, Winnie Nwagi, Rema Namakula, Nina Roz, Cindy Sanyu, Shebah Karungi lakini tuzo ya msanii bora wa kike kwenye tuzo za Janzi Awards mwaka wa 2021 zilimuendea Azawi. Ikumbukwe zaidi ya wasanii 300 waliteuliwa kushiriki kwenye tuzo za Janzi kwa mwaka wa 2021 ambapo kura 75,000 zilipigwa kwenye tuzo hizo ambazo ziliandaliwa kwa ajili ya kutambua mchango na kutoa heshima kwa wasanii wanaofanya vizuri kwenye tasnia ya muziki nchini Uganda.

Read More