TANASHA DONNA ADOKEZA UJIO WAKE MPYA

TANASHA DONNA ADOKEZA UJIO WAKE MPYA

Msanii wa muziki nchini Tanasha Donna ametangaza ujio wa ngoma yake mpya baada ya kimya cha muda mrefu bila kutoa hitsong yeyote. Tanasha ameweka wazi taarifa hiyo kwa mashabiki zake kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo amewataka mashabiki zake kukaa mkao wa kula kupokea wimbo wake mpya ambao ameutaja utatoka rasmi wiki ijayo. Mrembo huyo ambaye anaenda kuachia EP yake mpya baadae mwaka huu, kwa nyakati tofauti kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii amekuwa akidokeza juu ya ujio wake mpya. Ikumbukwe, ngoma yake ya mwisho kuitoa ilikuwa ni “Mood” ambayo ilitoka miezi 6 iliyopita na mpaka sasa ina zaidi ya views laki 4 kwenye mtandao wa Youtube.

Read More
 TANASHA DONNA ATHIBITISHA KUKAMILIKA KWA EP YAKE MPYA

TANASHA DONNA ATHIBITISHA KUKAMILIKA KWA EP YAKE MPYA

Nyota wa muziki nchini Tanasha Donna anaendelea kutupasha mapya kuhusu ujio wa EP yake mpya ambayo ana mpango wa kuiachia hivi karibuni. Katika mahojiano na mpasho  mkali huyo wa ngoma ya Complicationship amesema kwamba EP yake aliyoipa jina la This is me imekamilika kwa asilimia mia baada ya kuifanyia kazi kwa takriban mwaka mmoja na miezi mitatu. Tanasha ameenda mbali zaidi na kuwahakikishia mashabiki zake kwamba watarajie kupokea EP nzuri yenye jumla ya mikwaju 5 ya moto ambayo itazungumzia safari yake ya muziki wake. Hii ni EP ya pili kwa mtu mzima Tanasha Donna tangu aingie kwenye soko la muziki Afrika mashariki baada ya EP yake ya kwanza DONNA TELLA ya mwaka wa 2020 kufanya vizuri.

Read More
 TANASHA DONNA ARUSHA JIWE GIZANI , ASEMA HATOKUJA KULILIA PENZI LA DIAMOND PLATINUMZ

TANASHA DONNA ARUSHA JIWE GIZANI , ASEMA HATOKUJA KULILIA PENZI LA DIAMOND PLATINUMZ

Msanii wa kike nchini Tanasha Dona amefunguka na kudai kwamba hana muda wa kungangania penzi la mwanaume. Kupitia ukurasa wake wa Twittwer Tanasha amejinasibu kwa kusema kwamba atokuja kulilia penzi la mwanaume katika maisha yake huku akisisitiza kuwa ikitokea amejiaibisha mbele ya umma kwa kumgombania mwanaume mashabiki zake wamuadhibu juu ya hilo. Hitmaker huyo ngoma ya “Mood” amesema ana ufahamu mpana kuhusu suala la wanaume kuwaoa wanawake zaidi ya mmoja ila Mwenyezi Mungu anajua kwamba hatokujaa kuolewa kama mke wa pili kutokana na wivu alionao kwenye ishu ya mahusiano ya kimapenzi. Kauli Tanasha Donna imekuja mara baada ya walimwengu kwenye mitandao ya kijamii kumshinikiza alipiganie penzi la Baby Daddy wake Diamond Platinumz ambaye katika siku za hivi karibuni ameonekana akiwa karibu na Zuchu ambaye anadaiwa kuwa mpenzi mpya wa hitmaker huyo wa ngoma ya “Naanzaje”.

Read More
 PENZI LA TANASHA DONNA NA OMAH LAY  LAKOLEA MITANDAONI

PENZI LA TANASHA DONNA NA OMAH LAY LAKOLEA MITANDAONI

Moja kati ya headlines zinazo gonga vichwa vya habari mtandaoni ni issue inayomtaja mwanamuziki wa Nigeria Omah Lay kutoka kimapenzi na staa wa muziki nchini Tanasha Donna, sakata ambalo kila mtu analizungumzia katika namna yake. Katika nyakati tofauti tofauti kwa pamoja kupitia insta story zao kwenye mtandao wa Instagram Wawili hao wameshare picha zinazo onekana kushabihiana eneo moja ikiwemo hoteli wanaodaiwa kuwa wamekuwa wakijivinjari huko Mombasa huku wote wakipost kwenye muda unao tofautiana dakika moja tu. Vyanzo vya karibu na Tanasha, vinadai Hitmaker huyo wa “Gere” na Omah Lay wamekuwa pamoja mjini Mombasa tangu msanii huyo atue nchini Kenya jambo linalodaiwa kuwa lilimpelekea Omah Lay kususia kutumbuiza katika tamasha la Beach Fest  kwenye mkesha wa kuamkia mwaka mpya kutokana na kulewa na penzi la Tanasha Donna. Tetesi za Tanasha na Omah Lay kuwa kwenye mahusiano zilianza mwaka jana walipoonekana pamoja nchini Nigeria na Sudan Kusini wakiwa wanakula bata pamoja lakini pia walikuwa wakiachia comment za mahaba kwenye picha zao kwenye mtandao wa instagram jambo liliwaaminisha mashabiki kuna kitu kinaendelea kati yao. Hata hivyo hakuna mmoja kati yao amejitokeza kuthibitisha kama kweli wapo kwenye mahusiano ila ni jambo la kusubiriwa maana waswahili wana msemo wao unaosema penzi ni kikozi na halifichiki.

Read More
 TANASHA DONNA AFUNGUKA SABABU ZA KUPUNGUA KWA VIEWERS YOUTUBE

TANASHA DONNA AFUNGUKA SABABU ZA KUPUNGUA KWA VIEWERS YOUTUBE

Nyota wa muziki nchini Tanasha Donna amefunguka kuwa awali alilazimshwa kufanya mziki ambao hakumpenda ilipata watazamaji wengi wa haraka kwenye mtandao wa youtube. Kwenye kikao cha maswali na majibu aliyokuwa anafanya na mashabiki zake kwenye mtandao wa Instagram, Tanasha amesema kuwa sababu kuu ni kuwa amebadilisha aina ya mziki anaofanya na ni mziki anaopenda kando na alivyokuwa anafanya mziki wa awali kwa kulazimshwa. Kauli ya Tanasha donna inakuja mara baada ya Shabiki kuhoji iwapo anaridhika na jinsi mtandao wake wa youtube  ulivyo kwa sasa na ni kwanini nyimbo zake hazipati viwers wengi kama awali

Read More