Msanii Tory Lanez Afeli Kujaribu Kubatilisha Hukumu ya Jinai ya 2022

Msanii Tory Lanez Afeli Kujaribu Kubatilisha Hukumu ya Jinai ya 2022

Msanii wa muziki wa Marekani, Tory Lanez, ameshindwa katika jitihada zake za kuwasilisha ushahidi mpya ili kubatilisha hukumu yake ya jinai ya mwaka 2022. Lanez alifungua maombi mawili kuhusiana na shambulio la risasi lililotokea mwaka 2020 lililomkabili Megan Thee Stallion. Moja ya maombi hayo yalilenga kuanzisha hoja kwamba dereva wa mwendesha gari wa Peterson hakushuhudia kwenye kesi, huku lingine likitaka kuwasilisha tamko jipya kutoka kwa mlinzi wa Kelsey Harris, rafiki wa zamani wa karibu wa mwathiriwa. Hata hivyo, maombi yote mawili yamekataliwa Jumanne na Mahakama ya Rufaa ya California. Timu ya kisheria ya Lanez ilidai kwenye mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika Mei mwaka huu kwamba Bradley Jennings, aliyekuwa mlinzi na dereva wa Harris, alishuhudia mazungumzo ambapo Harris alidai kuwa ndiye aliyefatwa na bunduki na kuipiga mara kadhaa, na kwamba Peterson alishika mkono wake na hivyo bunduki ilipiga risasi zaidi. Lengo la ushahidi huo lilikuwa kuonesha kwamba bunduki ilipigwa risasi kwa bahati mbaya na si Lanez. Uamuzi wa mahakama kukataa ushahidi mpya unamaanisha kuwa Tory Lanez hatakuwa na nafasi ya kuutumia kama msingi wa kubatilisha hukumu yake. Kesi ya jinai ya mwaka 2022 hivyo inasalia thabiti, na msanii huyo sasa anakabiliana kikamilifu na athari za kisheria zinazotokana na makosa aliyopatikana nayo.

Read More
 Nicki Minaj Atishia Kufichua Ukweli kwa FBI na CIA Kufuatia Kisa cha Tory Lanez Kudungwa Kisu

Nicki Minaj Atishia Kufichua Ukweli kwa FBI na CIA Kufuatia Kisa cha Tory Lanez Kudungwa Kisu

Malkia wa muziki wa Hiphop duniani Nicki Minaj ameibua taharuki baada ya kudai kuwa anahisi tukio la Tory Lanez kudungwa kisu gerezani lilikuwa njama ya makusudi. Nicki sasa anasema yuko tayari kuzungumza na mashirika ya upelelezi ya Marekani, FBI na CIA, kuhusu kile anachodai kuwa ni mtandao wa vitisho vinavyohusisha watu wenye ushawishi mkubwa kwenye tasnia ya burudani. Nicki Minaj ameeleza kuwa maneno yaliyotolewa na MackWop, mshirika wa kundi la muziki la TDE, yanaonyesha wazi viashiria vya vitisho dhidi yake na vina uhusiano wa moja kwa moja na shambulio dhidi ya Tory. Aidha, amelaumu kile anachokiita ni tabia ya baadhi ya watu ndani ya tasnia ya muziki ambao wanajiona wako juu ya sheria na sasa wameanza kutoa vitisho hadharani. Tory Lanez, anayehudumia kifungo cha miaka 10 kwa kosa la kumpiga risasi msanii mwenza Megan Thee Stallion, alishambuliwa na kudungwa kisu mara 14 akiwa katika Gereza la Tehachapi, California, mwezi Mei 2025. Alipata majeraha mabaya ikiwemo mapafu kudidimia, pamoja na majeraha usoni, mgongoni na kichwani. Tukio hilo limezua maswali mengi kuhusu usalama wa wafungwa mashuhuri.

Read More
 Wakili wa Megan Thee Stallion Amshambulia Tory Lanez Baada ya Kuzindua Tovuti ya Kujitetea

Wakili wa Megan Thee Stallion Amshambulia Tory Lanez Baada ya Kuzindua Tovuti ya Kujitetea

Mvutano kati ya Megan Thee Stallion na Tory Lanez unaendelea kuchukua sura mpya, huku wakili wa Megan akitoa tamko kali kupitia jarida la XXL baada ya timu ya mawakili wa Tory kuzindua tovuti mpya inayodai kuonyesha ushahidi wa kutetea  haki ya msanii huyo. Tovuti hiyo, iliyoanzishwa na timu ya Tory Lanez, inalenga kushawishi umma kuhusu kutokuwa na hatia kwake katika kesi ya kumpiga risasi Megan Thee Stallion, tukio ambalo lilitokea mwaka 2020 na kumweka Tory kwenye matatizo makubwa ya kisheria. Katika kujibu hatua hiyo, wakili wa Megan alikemea vikali juhudi za Tory Lanez kujaribu kuandika upya simulizi ya tukio la kumpiga risasi Megan mwaka 2020. Alisema kuwa tovuti hiyo ni jaribio la kuwapotosha mashabiki na kulifanya jambo hili kuwa la burudani badala ya kutafuta haki. Wakili huyo alisisitiza kuwa Tory tayari alikutwa na hatia kupitia mfumo wa sheria wa Marekani, na kwamba kuendelea kujaribu kujiosha kupitia mitandao na vyombo vya habari ni kudhalilisha wahanga wa ukatili na kuleta mkanganyiko kwa umma. “Ni aibu kuona mtu anayejaribu kugeuza maumivu ya mtu kuwa kampeni ya mtandaoni. Ukweli ulishasemwa mahakamani, na haki ilitendeka,” ilisomeka sehemu ya taarifa hiyo. Kwa upande wa Tory Lanez, timu yake ya mawakili imeendelea kushikilia kuwa msanii huyo hakutenda kosa lolote, na wanasema tovuti hiyo ni jukwaa la kutoa taarifa walizoita “uhalisia wa tukio.” Wakati huu, Tory Lanez bado anahudumu kifungo baada ya kupatikana na hatia katika kesi hiyo. Hata hivyo, juhudi za timu yake za kupigania hadhi yake mbele ya macho ya umma zinaendelea kushika kasi, huku wafuasi wa pande zote wakiendelea kupambana mitandaoni kwa maoni na mitazamo tofauti.

Read More
 Amber Rose Aibua Mjadala Mpya Kuhusu Kesi ya Megan Thee Stallion

Amber Rose Aibua Mjadala Mpya Kuhusu Kesi ya Megan Thee Stallion

Mwanamitindo na mwanaharakati Amber Rose ameeleza hadharani sababu za kumtetea msanii Tory Lanez katika kesi ya kumpiga risasi Megan Thee Stallion mwaka 2020. Akizungumza kwenye mahojiano ya moja kwa moja katika kipindi cha Chris Cuomo kinachorushwa kupitia NewsNation, Rose alisema anaamini Lanez hana hatia na anastahili kusamehewa na Gavana wa California, Gavin Newsom. Katika mazungumzo hayo, Amber Rose alisisitiza kuwa ushahidi uliopo hauonyeshi moja kwa moja kuwa Tory ndiye alifyatua risasi. Alisema Lanez ameshathibitishwa kuwa hana uhusiano wa moja kwa moja na silaha iliyotumika, jambo linaloonyesha kuwa alipaswa kuachiliwa huru. Chris Cuomo, hata hivyo, aliibua hoja kuwa sampuli za DNA zilionyesha kuwa silaha hiyo ilikuwa inaweza kuguswa na watu wanne tofauti, lakini pia akaongeza kuwa Lanez alituma ujumbe wa kuomba msamaha baada ya tukio hilo, huku Megan Thee Stallion na rafiki yake Kelsey, waliokuwepo usiku huo, wakimtaja Lanez kama mtu aliyefyatua risasi. Amber Rose alijibu kwa kusema kuwa amesikia simulizi nzima kutoka kwa Tory Lanez mwenyewe, ambaye alimpigia simu moja kwa moja kutoka gerezani na kumueleza kile kilichotokea usiku huo. Kauli hii ya Amber Rose imezua maoni mseto mitandaoni, huku baadhi wakimtetea kwa kuonyesha huruma na kutaka haki ya kweli itendeke, huku wengine wakimtuhumu kwa kupuuza ushahidi wa upande wa Megan Thee Stallion. Haya yanakuja siku chache baada ya Amber Rose kuchapisha kipande cha video kinachomuonyesha Mwakilishi wa Bunge la Marekani, Anna Paulina, akimwambia Cuomo kuwa Tory Lanez hana hatia na kwamba kesi hiyo ililetwa kwake na Amber Rose mwenyewe.

Read More
 Rapa Tory Lanez Atajwa Kuanzisha Ugomvi Kabla ya Tukio la Kudungwa Kisu

Rapa Tory Lanez Atajwa Kuanzisha Ugomvi Kabla ya Tukio la Kudungwa Kisu

Mshukiwa wa tukio la kushambuliwa msanii wa muziki Tory Lanez, sasa amevunja ukimya, akidai alimdunga kisu  rapa huyo kwa sababu alihisi maisha yake yako hatarini. Kwa mujibu wa maafisa wa magereza, Tory Lanez alijeruhiwa vibaya kwa kudungwa kisu mara kadhaa akiwa gerezani, na mshambuliaji sasa anadai alikuwa akijilinda. Mshukiwa huyo ameeleza kuwa alisikia uvumi kuwa Tory Lanez alikuwa ameweka dau la kumuangamiza, jambo lililompelekea kuchukua hatua ya haraka ili kujinusuru. “Nilidhani Tory alikuwa amepanga kuniua. Nilisikia ametoa pesa kwa mtu yeyote aniondoe. Nililazimika kujihami,” alieleza katika mahojiano ya awali. Hata hivyo, mamlaka bado zinafanya uchunguzi ili kubaini ukweli wa madai hayo. Tory Lanez, ambaye anatumikia kifungo kwa kesi tofauti, alipata majeraha lakini inaripotiwa yuko katika hali thabiti baada ya tukio hilo. Tukio hili limezua maswali mengi kuhusu usalama wa wafungwa mashuhuri na hali halisi ya maisha ndani ya magereza ya Marekani. Mashabiki wa Tory Lanez wanaendelea kufuatilia maendeleo huku wengi wakitaka haki itendeke.

Read More
 Tory Lanez Ahamishwa Gerezani Baada ya Kudaiwa Kuchomwa Kisu Mara 14

Tory Lanez Ahamishwa Gerezani Baada ya Kudaiwa Kuchomwa Kisu Mara 14

Rapa Tory Lanez, ambaye jina lake halisi ni Daystar Peterson, ameripotiwa kuhamishwa kutoka Gereza la California Correctional Institution lililopo Tehachapi, baada ya tukio la kushambuliwa na kuchomwa kisu mara 14. Kwa mujibu wa vyanzo vya karibu na tukio hilo, Lanez alivamiwa ndani ya gereza hilo na kushambuliwa katika tukio linalodaiwa kuhusiana na migogoro ya magenge ya uhalifu, hasa kundi la Bloods. Ingawa majeraha aliyoyapata hayakuwa ya kutishia maisha, shambulio hilo limezua hofu kubwa kuhusu usalama wake akiwa gerezani. Baada ya tukio hilo, rapa huyo alihamishiwa katika Gereza la North Kern State Prison, lililoko Delano, California, kwa lengo la kumlinda dhidi ya mashambulizi zaidi. Uhamisho huo unatajwa kufanyika haraka mara baada ya shambulio hilo. Tory Lanez anatumikia kifungo cha miaka 10 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumpiga risasi msanii mwenzake Megan Thee Stallion mwaka 2020, tukio ambalo lilizua gumzo kubwa katika tasnia ya burudani ya Marekani. Hata hivyo, Idara ya Magereza na Marekebisho ya Tabia ya Jimbo la California haijatoa taarifa rasmi kuthibitisha tukio hilo au sababu za uhamisho, ikitaja sababu za faragha na usalama wa wafungwa. Mashabiki na wafuasi wa rapa huyo sasa wanasubiri taarifa rasmi kuhusu hali yake ya afya na hatima ya kesi au uchunguzi wowote unaoweza kufunguliwa kutokana na tukio hilo la kushangaza.

Read More
 Wanasheria wa Megan Thee Stallion Wakanusha Ushahidi Mpya Katika Kesi ya Tory Lanez

Wanasheria wa Megan Thee Stallion Wakanusha Ushahidi Mpya Katika Kesi ya Tory Lanez

Wakili wa rapa maarufu Megan Thee Stallion wametoa taarifa rasmi wakikanusha madai ya kambi ya Tory Lanez kuwa kuna ushahidi mpya ambao unaweza kumuondolea hatia kwenye kesi ya kumpiga risasi Megan mwaka 2020. Katika ripoti yenye kurasa 31 iliyotolewa wiki hii, timu ya sheria ya Megan imeeleza kuwa madai hayo yanayosambazwa ni ya kupotosha na hayana msingi wowote wa kisheria. Wameyataja kama “hadithi za uongo” zinazoenezwa na kile walichokiita “watesi wajinga.” “Hakuna ushahidi mpya kutoka Ring camera kama inavyodaiwa, na shahidi anayetajwa hajawahi kuwa eneo la tukio, wala kutoa ushahidi wowote hadharani au mahakamani,” alisema wakili Alex Spiro. Megan Thee Stallion pia aliunga mkono msimamo huo mapema wiki hii, akitoa kauli zinazosisitiza kuwa juhudi za kudhoofisha ukweli ni sehemu ya mateso yanayoendelea dhidi yake kama mhanga wa tukio hilo. Kesi hiyo iliibua hisia kali za kijamii na mitandaoni, na licha ya hukumu ya mahakama, juhudi za upande wa Tory Lanez kutaka kesi ifunguliwe upya au hukumu ipunguzwe zimeendelea kuchochea mijadala. Hata hivyo, timu ya Megan inasisitiza kuwa hakuna msingi wa kisheria au ushahidi wowote mpya wa kuanzisha mwelekeo tofauti wa kisheria. Kwa sasa, Tory Lanez anatumikia kifungo gerezani kufuatia hukumu hiyo ya kumpiga risasi Megan, na kesi hiyo inaendelea kuibua mazungumzo kuhusu haki kwa waathirika wa vurugu za silaha, na pia athari za upotoshaji wa umma kwenye kesi nyeti.

Read More
 Megan Thee Stallion Aonyesha Hasira kwa Mashabiki wa Tory Lanez Walio na Mashaka Kuhusu Kesi ya Risasi

Megan Thee Stallion Aonyesha Hasira kwa Mashabiki wa Tory Lanez Walio na Mashaka Kuhusu Kesi ya Risasi

Rapa maarufu kutoka Marekani, Megan Thee Stallion, ameamua kupambana hadharani na mashabiki wa Tory Lanez ambao bado wanakanusha ukweli kwamba mwanamuziki huyo alimpiga risasi licha ya uamuzi wa mahakama ya juri mjini Los Angeles kuthibitisha hilo. Kupitia ujumbe wake kwenye mitandao ya kijamii, Megan ameonesha kuchoshwa na mashambulizi ya mfululizo kutoka kwa baadhi ya watu wanaoendeleza kampeni ya kumdhalilisha, huku akimtaja Tory Lanez kama shetani anayeendelea kumletea mateso hata baada ya hukumu. “Muda umefika muache kunitesa. Mlikuwa na nafasi ya kusema mliyotaka mahakamani. Mnaendelea tu na uongo  ni kama mapepo,” Megan alisema kwa hasira. Megan ambaye anaendelea na kazi yake ya muziki, ameweka wazi kuwa bado anapitia changamoto za kiakili kutokana na matukio hayo, hasa kutokana na mashambulizi ya mfululizo kutoka kwa baadhi ya watu mitandaoni. Ameongeza kuwa bado anaumizwa na namna watu wanavyopuuza ukweli na kumshambulia yeye badala ya kumwajibisha Tory. “Mahakama ilizungumza. Ukweli ulidhihirika. Lakini bado naandamwa kana kwamba mimi ndiye mwenye makosa.” aliongeza. Kauli hiyo imeibua mjadala mkali mtandaoni huku mashabiki wake wakimtetea vikali na kuitaka jamii kumheshimu kama manusura wa tukio la vurugu. Wengine, hususan wafuasi wa Tory, bado wanaonekana kushikilia imani tofauti, jambo linalozua sintofahamu kubwa. Tory Lanez tayari anatumikia kifungo gerezani baada ya kupatikana na hatia ya kumpiga Megan risasi mwaka 2020, tukio lililotokea baada ya sherehe usiku. Huu ni mwendelezo wa mvutano kati ya Megan na Tory ambao umegusa si tu mashabiki wao, bali pia wasanii na wanaharakati wa haki za wanawake kwenye tasnia ya muziki duniani.

Read More
 Ombi la Kumtaka Gavana Newsom Kumsamehe Tory Lanez Lavuka Saini 250,000

Ombi la Kumtaka Gavana Newsom Kumsamehe Tory Lanez Lavuka Saini 250,000

Msanii maarufu wa muziki wa Hip Hop, Tory Lanez, ameendelea kupata uungwaji mkono mkubwa mtandaoni kupitia ombi lililowekwa kwenye mtandao wa Change.org, likimtaka Gavana wa California, Gavin Newsom, amsamehe. Kwa siku tatu mfululizo, ombi hilo limekuwa namba moja kwa kupendwa na kusainiwa zaidi kwenye jukwaa hilo, na kufikisha zaidi ya saini 250,000. Ombi hilo linataka msamaha rasmi kwa Tory Lanez kufuatia kifungo alichopokea baada ya kupatikana na hatia ya kumjeruhi rapa Megan Thee Stallion kwa risasi. Juhudi hizo zimeungwa mkono na watu maarufu kutoka tasnia ya burudani nchini Marekani, akiwemo Drake, Amber Rose, na Ty Dolla Sign. Wanaounga mkono ombi hilo wanadai kuwa hukumu dhidi ya Tory ilikuwa na upendeleo na kwamba anastahili kupewa nafasi ya pili. Hata hivyo, kuna kundi linalopinga hatua hiyo, likisema kuwa kila mtu anapaswa kuwajibika kwa matendo yake bila kujali umaarufu. Hadi kufikia sasa, ofisi ya Gavana Newsom haijatoa tamko rasmi kuhusu ombi hilo au uwezekano wa msamaha. Hali ikiendelea kuchacha, mjadala kuhusu haki, sheria, na nafasi ya watu maarufu mbele ya vyombo vya sheria unaendelea kushika kasi.

Read More
 Mwanasheria wa Megan Thee Stallion Avunja Ukimya Kufuatia Madai Mapya ya Timu ya Tory Lanez

Mwanasheria wa Megan Thee Stallion Avunja Ukimya Kufuatia Madai Mapya ya Timu ya Tory Lanez

Mwanasheria wa mwanamuziki maarufu wa Marekani, Megan Thee Stallion, Alex Spiro, amejitokeza kutoa kauli kali kufuatia taarifa zilizotolewa jana na timu ya mawakili wa Tory Lanez kuhusu kesi ya kumpiga risasi Megan. Kupitia taarifa kwa jarida la XXL Magazine, Spiro amejibu madai yaliyotolewa katika mkutano wa waandishi wa habari uliandaliwa na mawakili wa Lanez, ambapo walidai kuwa rafiki wa Megan, Kelsey Harris, ndiye aliyempiga risasi msanii huyo – na siyo Tory Lanez kama ilivyodaiwa awali. Spiro amekanusha vikali madai hayo, akisisitiza kuwa hukumu iliyotolewa dhidi ya Tory Lanez ilifuata mchakato halali wa kisheria.  “Tory Lanez alishtakiwa na kutiwa hatiani na wenzake, na kesi yake ilipitia katika mfumo sahihi wa mahakama. Hili si suala la kisiasa – hii ni kesi ya shambulio la kikatili ambalo lilisikilizwa na kuamuliwa kwa mujibu wa sheria,” alisema Spiro. Kesi hiyo, ambayo ilivuta hisia za watu wengi kote duniani, ilimalizika kwa Tory Lanez kupatikana na hatia ya kumshambulia Megan kwa kutumia silaha ya moto, tukio lililotokea Julai 2020. Hukumu hiyo ilileta mgawanyiko mkubwa mtandaoni kati ya mashabiki wa pande zote mbili. Kwa sasa, bado haijabainika kama ushahidi mpya uliodaiwa na timu ya Tory Lanez utawasilishwa rasmi mahakamani kwa ajili ya rufaa au mapitio ya kesi.

Read More
 Mlinzi Avunja Ukimya: Afichua Ukweli Mpya Kuhusu Kesi ya Tory Lanez

Mlinzi Avunja Ukimya: Afichua Ukweli Mpya Kuhusu Kesi ya Tory Lanez

Timu ya mawakili ya rapa Tory Lanez imetangaza habari mpya inayoweza kubadili mwelekeo wa kesi yake. Katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika tarehe 14 Mei 2025, mawakili wa Lanez walidai kuwa mlinzi wa Kelsey Harris, Bradley James, ambaye alifanya kazi na Kelsey wakati wa kesi ya awali ya Lanez, sasa anadai kuwa alisikia Kelsey akisema kuwa yeye ndiye aliyefyatua risasi dhidi ya Megan Thee Stallion mnamo Julai 15, 2020. Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mawakili wa Tory, Bradley James amekiri kwamba alisikiliza kwa simu mazungumzo ambapo Kelsey alikiri kumpiga risasi Megan. James alidai pia kuwa Tory Lanez alijaribu tu kuondoa bunduki mikononi mwa Kelsey baada ya yeye kufyatua risasi tatu kwa Megan. “Ushahidi huu mpya unaendelea kuthibitisha kuwa Bwana Peterson hakumpiga risasi Bi. Pete,” alisema Water Roberts, mshauri wa kisheria wa timu ya Unite the People, mbele ya waandishi wa habari. “Tory Lanez hakuhusika katika tukio hili la kinyama.” Taarifa hizi zinakuja wakati ambapo Tory Lanez anaendelea kupona hospitalini baada ya kudaiwa kushambuliwa kwa kisu gerezani mnamo Mei 12, 2025. Kupitia ushahidi huu mpya, timu ya mawakili ya Lanez sasa inadai kuwa adhabu ya kifungo cha miaka 10 inayomkabili inapaswa kupunguzwa au hata kufutwa kabisa. Kwa upande mwingine, Jarida la XXL iliwasiliana na mawakili wa Kelsey Harris na timu ya Megan Thee Stallion ili kupata maoni yao kuhusu madai haya mapya, lakini hadi sasa hawajatoa tamko rasmi. Kesi hii ya Tory Lanez imekuwa ikivutia umakini mkubwa kutoka kwa umma na wadau wa muziki, na ushahidi huu mpya unaleta maswali mengi kuhusu haki na ukweli wa matukio yaliyojiri mwaka 2020. Muda utaonyesha kama haya mapya yataweza kubadilisha hatima ya Lanez.

Read More
 Chris Brown Amkingia Kifua Tory Lanez, Wadau Wahoji Nia Yake Halisi

Chris Brown Amkingia Kifua Tory Lanez, Wadau Wahoji Nia Yake Halisi

Staa wa muziki kutoka Marekani Chris Brown ameendelea na juhudi zake za kumtetea msanii Tory Lanez, ambaye anahusishwa na tukio la kupigwa risasi mguu wa rapa Megan Thee Stallion. Katika hatua ya hivi karibuni, Kupitia ujumbe aliouandika kwenye Insta-stori, Chris alisisitiza kuwa Tory Lanez anapaswa kuachiliwa kutokana na kile alichokiita udhalimu wa kifungo kisichostahili. Hatua hii imezua maswali na mjadala miongoni mwa mashabiki na wadadisi wa tasnia ya muziki, huku wengine wakijiuliza ikiwa Chris anafanya hivi kwa nia ya kumsaidia Tory au kama ni hatua ya kurejesha heshima yake mwenyewe. Katika ujumbe wake, Chris alikiri kumsaidia Tory Lanez kifedha wakati alikumbwa na changamoto za kiuchumi, jambo ambalo lilizua maswali kuhusu uhusiano wa kifamilia na mshikamano kati ya wanamuziki hawa wawili. Katika muktadha huu, baadhi ya watu wanaona hatua ya Chris Brown kama njia ya kuonyesha uaminifu kwa Tory, ambaye anahusishwa na mashitaka ya kumpiga risasi Megan Thee Stallion miaka miwili iliyopita. Hata hivyo, kuna wengi wanaopinga msimamo wa Chris, wakisema kwamba hatua hii inakosa muktadha wa kijamii na kisheria, na kwamba kumtetea Tory Lanez kunashindwa kuzingatia athari za matendo hayo kwa Megan, ambaye alikumbwa na jeraha kubwa katika tukio hilo. Mashabiki na wadadisi wengi wanaona kuwa Chris anajikuta akikwepa dhamira ya maadili ya kijamii kwa kumtetea msanii ambaye, kwa kiasi kikubwa, ameonyesha kuwa na matatizo makubwa ya kijamii. Kwa sasa, msimamo wa Chris Brown unaendelea kuwa na maoni mseto miongoni mwa mashabiki na waandishi wa habari, huku mashabiki wa Megan Thee Stallion na wanaharakati wakionyesha hasira dhidi ya mtu yeyote anayeonekana kupuuza athari za unyanyasaji wa kijinsia. Hii ni kwa sababu mzozo huu wa kisheria umekuja wakati ambapo jamii inazidi kujikita katika kulinda haki za waathirika wa unyanyasaji na kupinga vitendo vya aina hii.

Read More