TMZ Yaanika Picha ya Mfungwa Anayedaiwa Kumchoma Kisu Rapa Tory Lanez Jela

TMZ Yaanika Picha ya Mfungwa Anayedaiwa Kumchoma Kisu Rapa Tory Lanez Jela

Mtandao wa burudani wa TMZ umechapisha picha ya mfungwa anayeitwa Santino Casio, anayeshukiwa kumshambulia kwa kisu rapa Tory Lanez akiwa gerezani. Kwa mujibu wa TMZ, Casio anatumikia kifungo cha maisha gerezani kwa kosa la mauaji na anatajwa kuwa na historia ya matukio ya vurugu tangu alipoanza kutumikia kifungo chake. Tukio hilo la kushangaza liliripotiwa kutokea siku ya Jumatatu saa 1:20 asubuhi (7:20 a.m) katika gereza la North Kern, California, ambapo Tory Lanez alishambuliwa na kuchomwa kisu mara 14 kwenye maeneo mbalimbali ya mwili wake ikiwemo kichwani, kifuani, na mgongoni. Chanzo cha karibu na tukio hilo kimeripoti kuwa Tory aliwekwa kwenye mashine ya kupumua mara baada ya tukio kutokana na majeraha makubwa, lakini taarifa za hivi karibuni zinaeleza kuwa anaendelea vizuri akiwa katika Hospitali ya North Kern Medical Center. Tukio hili limeibua maswali kuhusu usalama wa wafungwa maarufu ndani ya magereza ya Marekani, hasa ikizingatiwa kuwa Santino Casio anatajwa kuwa tayari amehusika katika matukio mengine ya fujo akiwa jela. Tory Lanez, ambaye anatumika kifungo cha miaka 10 gerezani baada ya kupatikana na hatia ya kumpiga risasi mwanamuziki Megan Thee Stallion mnamo Julai 2020, huenda sasa akahamishwa kutoka gereza hilo kwa ajili ya usalama wake. Ripoti zinaonyesha kuwa endapo atarejeshwa tena North Kern, ulinzi wake utaimarishwa kwa kiwango cha juu zaidi. Hadi sasa, mamlaka ya magereza bado haijatoa taarifa rasmi kuhusu sababu ya shambulio hilo au hatua zitakazochukuliwa dhidi ya Santino Casio.

Read More
 Tory Lanez Ajeruhiwa Vibaya Gerezani, Inadaiwa Alichomwa Visu Mara 14

Tory Lanez Ajeruhiwa Vibaya Gerezani, Inadaiwa Alichomwa Visu Mara 14

Msanii wa muziki kutoka Canada, Tory Lanez, anaripotiwa kujeruhiwa vibaya baada ya kushambuliwa gerezani, akidaiwa kuchomwa visu mara 14 na mtu anayedaiwa kuwa mwanachama wa genge hatari la kihuni kutoka Mexico. Kwa mujibu wa sauti inayosambaa mitandaoni ya Wack 100, mmoja wa watu wenye ushawishi mkubwa katika tasnia ya burudani na anayejulikana kwa mara kwa mara kudai kuwa na taarifa za ndani, genge hilo la kihuni la Mexico linahusishwa na shambulio hilo la kushangaza lililotokea katika Gereza la North Kern, nchini Marekani. Katika sauti hiyo, Wack 100 anasikika akisema:  “Walimkamata Tory Lanez ndani. Nasikia alichomwa mara 14. Hili ni genge la kihuni kutoka upande wa Kusini mwa mpaka. Jamaa wana msimamo mkali, na wakimlenga mtu, si mchezo.” Ingawa hakutaja jina la chanzo chake wala kutoa ushahidi wa moja kwa moja, Wack 100 alionya kuwa tukio hilo linaweza kuchochea mzozo mkubwa baina ya makundi ya kihalifu ndani ya gereza hilo. Hadi sasa, sababu rasmi ya shambulio hilo haijabainishwa, huku uchunguzi ukiendelea kufanywa na mamlaka husika. Mamlaka za magereza zimethibitisha kwamba tukio la vurugu lilitokea katika gereza hilo na kwamba mmoja wa wafungwa alijeruhiwa vibaya. Hata hivyo, hawakutaja jina la Tory Lanez wala kueleza undani wa shambulio hilo kwa wakati huu. Vyanzo vya karibu na kesi hiyo vinaeleza kuwa huenda msanii huyo akahamishiwa kwenye gereza jingine kwa sababu za kiusalama. Mashabiki wake pamoja na watu mashuhuri kwenye mitandao ya kijamii wameonyesha wasiwasi mkubwa kuhusu hali ya Tory, wakisubiri tamko rasmi kutoka kwa mawakili wake au familia yake.

Read More
 Tory Lanez adaiwa kupitia nyakati ngumu zaidi katika maisha yake

Tory Lanez adaiwa kupitia nyakati ngumu zaidi katika maisha yake

Rapa kutoka nchini Canada Tory Lanez, amedaiwa kupitia nyakati ngumu sana kwenye maisha yake na anajutia kwanini hakukiri makosa yake Mahakamani mwezi Disemba. Tovuti ya Rolling Stone imeandika taarifa hiyo wakati Tory Lanez akiwa rumande kwa sasa akisubiri hukumu yake ambayo itasomwa Februari 28 mwaka huu ambapo huenda akahukumiwa kifungo cha miaka 22 na miezi 8 Jela. Utakumbuka Tory Lanez alikutwa na hatia ya makosa matatu ikiwemo la kumshambulia na kumjeruhi kwa risasi aliyekuwa mpenzi wake mwanamuziki Megan Thee Stallion.

Read More
 Familia ya Rapa Tory Lanez yamsameha Megan Thee Stallion

Familia ya Rapa Tory Lanez yamsameha Megan Thee Stallion

Familia ya rapa Tory Lanez imeweka wazi kumsamehe rapa Megan Thee Stallion. Baba mzazi wa rapa Tory Lanez, Sostar Peterson amethibitisha hilo kufuatia sakata la mwanae kukutwa na hatia ya makosa ya kumpiga risasi ya mguu rapa huyo Julai, mwaka 2020.. Kauli ya mzee huyo imekuja wiki chache baada ya kutoridhishwa na uamuzi wa Mahakama juu ya mwanae ambapo aliishtumu label ya Roc Nation ya Jay Z kuhusika katika uamuzi huo wa Mahakama. Ikumbukwe, Tory Lanez alikutwa na hatia ya makosa yote matatu na kwa sasa yupo rumande akisubiri hukumu yake kusomwa Februari 28, mwaka 2023 akitazamia kifungo cha miaka 22 jela.

Read More
 Tarehe ya hukumu ya Tory Lanez yasogezwa mbele

Tarehe ya hukumu ya Tory Lanez yasogezwa mbele

Hukumu ya Tory Lanez imesogezwa mbele kutoka Januari 27 na sasa itatoka Februari 28 mwaka huu. Wiki iliyopita Tory Lanez alimfukuza kazi mwanasheria wake na kumuajiri mpya (David Kenner) ambaye ana uzoefu na mashtaka ya jinai. wakili huyo “David Kenner” ambaye ana uzoefu katika kesi za jinai aliwahi pia kumsaidia rapa Snoop Dogg kwenye kesi yake ya mauaji mwaka 1993. Utakumbuka mwaka jana Tory alikutwa na hatia ya makosa yote matatu ambapo kifungo chake ni zaidi ya miaka 22 jela. Tory Lanez hadi sasa amebaki rumande akisubiri hukumu yake ambayo itasomwa Februari 28, mwaka 2023.

Read More
 Tory Lanez amfuta kazi mwanasheria wake

Tory Lanez amfuta kazi mwanasheria wake

Mitandao mbalimbali ya nchini Marekani imeripoti kwamba Rapa Tory Lanez amemfukuza kazi Mwanasheria wake na kumuajiri David Kenner ambaye ana uzoefu mkubwa. David Kenner anatajwa kuwawakilisha wasanii na watu maarufu kwenye Kesi zao kubwa ikiwemo ile ya Suge Knight, CEO wa zamani wa Label ya Death Row. Lakini watalaamu wa masuala ya sheria wanasema, inaweza kuwa sio muda sahihi kwa Kenner kuweka mguu wake kwenye Kesi ya Tory Lanez kwani amechelewa sana, Kabla ya Mahakama kumkuta na hatia ndio ungekuwa muda mzuri zaidi. Tory Lanez ambaye yupo rumande kwa sasa, mahakama itatoa hukumu ya kesi yake Januari 27 mwaka huu hii ni baada ya kukutwa na hatia kumpiga risasi Megan Thee Stallion.

Read More
 Mashabiki wa Tory Lanez waanzisha ombi kukataa rufaa ya kesi yake dhidi ya Megan Thee Stallion

Mashabiki wa Tory Lanez waanzisha ombi kukataa rufaa ya kesi yake dhidi ya Megan Thee Stallion

Mashabiki wa Rapa Tory Lanez, wameanzisha kampeni ya kushinikiza ombi la kukataa rufaa baada ya kutoridhishwa na maamuzi ya mahakama kwa rapa huyo katika kesi yake ya kumshambulia risasi Megan Thee Stallion Julai mwaka 2020. Mpaka sasa ombi hilo limefikisha zaidi ya saini 30,000 . Hatua hii imekuja siku chache kufuatia ya timu ya Tory Lanez kuonekana kutoridhishwa na maamuzi ya mahakama, ambapo wakili wake George Mgdesyan alidai anapanga kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo kwani hakuna ushahidi uliojitosheleza. Tory Lanez atabaki rumande akingoja hukumu yake kusomwa Januari 27, mwaka 2023 baada ya kukutwa na hatia kwenye mashtaka matatu ikiwemo kumshambulia Megan kwa kutumia silaha lakini pia kubeba silaha iliyopakiwa risasi na ambayo pia haijasajiliwa.

Read More
 Tory Lanez afunguka baada ya mahakama kumpata na hatia ya kumjeruhi Megan Thee Stallion

Tory Lanez afunguka baada ya mahakama kumpata na hatia ya kumjeruhi Megan Thee Stallion

Rapa Tory Lanez, amefunguka kwa mara ya kwanza baada ya mahakama kumpata na hatia kwenye shtaka la kumpiga risasi Megan Thee Stallion, Julai mwaka 2020. Kwa mujibu wa L.A Times, rapa huyo amekaririwa akisema kuwa amesikitishwa na uamuzi wa mahakama lakini anaamini kila jambo katika maisha lina sababu zake. Tory Lanez atabaki rumande akingoja hukumu yake kusomwa Januari 27, mwaka 2023 baada ya kukutwa na hatia kwenye mashtaka matatu ikiwemo kumshambulia Megan kwa kutumia silaha lakini pia kubeba silaha iliyopakiwa risasi na ambayo pia haijasajiliwa. Hata hivyo timu ya Tory Lanez imeonekana kutoridhishwa na maamuzi ya mahakama, hivyo wakili wake George Mgdesyan anapanga kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo kwani hakuna ushahidi uliojitosheleza.

Read More
 Tory Lanez akutwa na hatia ya kumpiga risasi Megan Thee Stallion

Tory Lanez akutwa na hatia ya kumpiga risasi Megan Thee Stallion

Mahakama ya jiji la Los Angeles imemkuta na hatia rapa Tory Lanez kwa makosa matatu ikiwemo la kumshambulia na kumjeruhi kwa risasi aliekuwa mpenzi wake mwanamuziki Megan Thee Stallion. Tukio hilo lilitokea baada ya mabishano yaliyosababishwa na utani ambapo inadaiwa Tory Lanez alikasirika na kufyatua risasi zilizomjeruhi miguuni Megan Thee Stallion. Mara baada ya maamuzi ya mahakama Lanez aliondoka mahamani hapo chini ya ulinzi mkali kuelekea gereza la Los Angeles kusubiri kuanza kutumikia adhabu yake. Tory Lanez ambaye jina lake ni Daystar Peterson anaweza kuhukumiwa kifungo cha mpaka miaka 22 jela katika hukumu inayotarajiwa kusomwa Januari 25.

Read More
 Tory Lanez awekwa kifungo cha ndani kufuatia kumshambulia August Alsina

Tory Lanez awekwa kifungo cha ndani kufuatia kumshambulia August Alsina

Mwanamuziki Tory Lanez amewekwa Kifungo cha ndani (House Arrest) kufuatia sakata lake la kumshambulia August Alsina mapema mwezi uliopita. Jaji amesema kwa kitendo kile, Tory Lanez ameharibu masharti ya dhamana kwenye shtaka lake dhidi ya Megan Thee Stallion. Lanez atakuwa chini ya uangalizi wa kifungo cha ndani kutokana na sababu zilizotolewa na waendesha mashtaka kwamba amekuwa mtu hatari kwenye Jamii, na atakaa hadi pindi Kesi yake ya kumpiga risasi Megan Thee Stallion ikianza kusikilizwa, November 28 mwaka huu.

Read More
 Tory Lanez alia na uongo wa wanawake, awataka wanaume wawe makini

Tory Lanez alia na uongo wa wanawake, awataka wanaume wawe makini

Staa wa muziki kutoka Marekani Tory Lanez ametoa angalizo kwa wanaume wawe makini na wadada wa karne hii kwa kuwa ni waongo kupitiliza. Kupitia ukurasa wake wa Twitter Tory Lanez amewataka wanaume kutowaamini wasichana haswa kwenye masuala ya mapenzi. “Baadhi ya wasichana wanaweza kukufanya uhisi kwamba wanaweza kujiua kama utaachana nao. Niko hapa kuwaambia washkaji zangu Mwanamke hawezi kujitoa uhai, Hiyo hali itamuondoka tu Jiokoe mwenyewe”, Ameandika. Hata hivyo hajajulikana ni kitu gani kimemfanya rapa huyo kutoa kauli hiyo yenye ukakasi ila walimwengu wamehoji huenda kuna mwanamke amepiga tukio la mwaka kwenye mahusiano yake kiasi cha kumuacha na makasiriko ya kuvunjwa moyo.

Read More
 TORY LANEZ AKANUSHA KUMPIGA AUGUST ALSINA

TORY LANEZ AKANUSHA KUMPIGA AUGUST ALSINA

Mwanamuziki kutoka Marekani August Alsina amedai kwamba amepigwa na kuumizwa vibaya na Tory Lanez. Kwa mujibu wa andiko lake kwenye mtandao wa instagram, Alsina amesema Tory alimshambulia wakati akiondoka kwenye onesho moja mjini Chicago Juzi Jumamosi. Jana Jumapili mwimbaji huyo wa R&B ali-posti picha ambazo zinamuonesha akivuja damu mdomoni na kuelezea tukio hilo kwamba Lanez alimfuata akiwa na walinzi 8 huku yeye akiwa hana ulinzi wowote. Kwenye maelezo yake, Alsina anasema alishambuliwa na Tory Lanez baada ya kutompa mkono kama ishara ya kusalimiana kwa kuwa alifuata masharti ya madaktari wake kutopeana mikono kiholela. Tory Lanez naye amejibu kwa kukanusha taarifa hizo ambapo kupitia insta story yake, amedai siku hiyo hakuwepo eneo hilo na alikuwa studio akifanya kazi zake.

Read More