Mtoto Aonyesha Upendo kwa Muziki wa Toxic Lyrikali kwa Kuchana “Long Story” Bila Kukwama

Mtoto Aonyesha Upendo kwa Muziki wa Toxic Lyrikali kwa Kuchana “Long Story” Bila Kukwama

Shabiki mdogo wa muziki ameibua mshangao na furaha mitandaoni baada ya kuonyesha kipaji chake cha kipekee kwa kuuchana wimbo maarufu wa rapa Toxic Lyrikali, Long Story, bila kukosea hata mstari. Clip ya video inayomuonyesha mtoto huyo ikisindikiza mashairi ya wimbo huo kwa ustadi mkubwa imeenea kwa kasi, jambo lililowagusa mashabiki wengi wa hip hop na kumfanya avune sifa tele. Mashabiki wengi wamepongeza hatua ya mtoto huyo, wakisema ni ishara ya namna muziki wa Toxic Lyrikali unavyowagusa hata vijana wadogo. Baadhi wamesema kitendo hicho kinadhihirisha jinsi muziki unaweza kuvuka vizuizi vya umri na kuwa chombo cha kuunganisha watu. Wimbo Long Story, uliotolewa miezi sita iliyopita, umeendelea kufanya vizuri kwenye majukwaa ya kidigitali ukiwa na zaidi ya watazamaji milioni moja kwenye YouTube. Toxic Lyrikali, ambaye amejizolea mashabiki kutokana na uandishi wake wa kina na uwasilishaji wa hisia halisi, amekuwa akitambulika kama mmoja wa wakali wa rapa wa kizazi kipya nchini Kenya.

Read More
 Rapa Toxic Lyrikali Awajibu Wakosoaji Baada ya Kumtawaza Rais Ruto kwa Muhula wa Pili

Rapa Toxic Lyrikali Awajibu Wakosoaji Baada ya Kumtawaza Rais Ruto kwa Muhula wa Pili

Rapa mwenye utata, Toxic Lyrikali, amewajibu vikali wakosoaji wake mitandaoni wanaomuita msaliti, kufuatia hatua yake ya kumtawaza Rais William Ruto kuhudumu kwa muhula wa pili katika hafla iliyofanyika Ikulu ya Nairobi. Kupitia Instagram Live, msanii huyo amesisitiza kuwa hana muda wa kujibizana na wakosoaji, akieleza kuwa kwa sasa anataka kufurahia matunda ya kazi yake ya muziki.. Hitmaker huyo wa Backbencher, ameongeza kuwa hatatishwa na maneno ya kejeli dhidi yake, akieleza kuwa maisha ya tabu na raha yamekuwa sehemu ya safari yake ya muziki, hivyo hawezi kuyumbishwa na maneno ya wafuasi wake. Aidha, rapa huyo amewataka wakosoaji wake kuacha kufuatilia maisha yake binafsi na badala yake wazingatie shughuli zinazoweza kuwapatia riziki. Hata hivyo, msanii huyo kwa sasa anatuhumiwa na baadhi ya mashabiki kuwa na kiburi na pia kuwasaliti vijana, hasa kwa kuonyesha uhusiano wa karibu na serikali ya Rais Ruto, ambayo imekuwa ikikumbana na upinzani mkubwa hasa kutoka kwa vijana mitandaoni.

Read More
 Parroty Afufua Bifu na Toxic Lyrikali Kupitia Picha ya Siri

Parroty Afufua Bifu na Toxic Lyrikali Kupitia Picha ya Siri

Msanii wa muziki wa gengetone, Parroty Vunulu, amezua gumzo mitandaoni baada ya kuwaomba mashabiki wake kumsaidia kutambua picha ya mwanaume asiyejulikana ambaye amekuwa akijitokeza mara kwa mara kwenye sehemu ya maoni ya mitandao yake ya kijamii. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Parroty aliahidi kumpa zawadi ya KSh 1,000 shabiki atakayefanikisha kumtambua mwanaume huyo. Ingawa hakumtaja moja kwa moja, mashabiki wengi wamehusisha picha hiyo na rapa Toxic Lyric Kali, anayejulikana kwa wimbo Backbencher. Inadaiwa kuwa Parroty na Toxic Lyric Likali hawako kwenye uhusiano mzuri baada ya madai kwamba rapa huyo alimuaibisha Parroty mtandaoni alipomwomba kufanya kolabo. Tukio hili limeendeleza mvutano wa chini kwa chini kati ya wasanii hao, huku mashabiki wakisubiri kuona kama Toxic Lyrikali.

Read More
 Toxic Lyrikali Ajibu Wakosoaji Wanaodai Ana Kiburi

Toxic Lyrikali Ajibu Wakosoaji Wanaodai Ana Kiburi

Msanii wa Hip Hop nchini Kenya, Toxic Lyrikali, ameibua gumzo mtandaoni baada ya kuwajibu vikali wakosoaji wanaodai kuwa ana kiburi. Kupitia mitandao ya kijamii, msanii huyo alionekana kukerwa na lawama hizo, akisema kuwa watu wanaomuita mkiburi hawafahamu muktadha wa ujumbe wake. “Wenye wanasema niko na kiburi wanaskizanga bongo,” Toxic aliandika. Kauli hiyo imewagawa mashabiki wake, huku baadhi wakimtetea wakisema anazungumza kwa uhalisia, na wengine wakimshutumu kwa majivuno na dharau kwa wasanii wachanga. Kauli hii imekuja siku mbili tu baada ya msanii huyo kuwashauri wasanii chipukizi kutomlipa pesa kwa ajili ya kufanya collabo naye, bali waitumie hiyo hela kujiendeleza kimuziki “Pesa unataka kunipea ya collabo, fanya nayo do ba deadly,” aliandika instagram. Kauli hizi zimezua mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii, huku baadhi ya mashabiki wakimtetea kwa kusema anazungumza ukweli mgumu ambao wengi wanaogopa kusema, huku wengine wakimshutumu kwa majivuno na kuwakandamiza wasanii wachanga.

Read More
 Toxic Lyrikali Apata Baraka za Nyashinski Baada ya Mafanikio ya ‘Cartman’ YouTube

Toxic Lyrikali Apata Baraka za Nyashinski Baada ya Mafanikio ya ‘Cartman’ YouTube

Msanii nyota wa muziki wa hip hop nchini Kenya, Nyashinski, ameonyesha wazi kuunga mkono na kubariki kazi ya rapper chipukizi Toxic Lyrikali kupitia wimbo wake mpya uitwao “Cartman”. Kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii, Nyashinski alielezea kuvutiwa na ubunifu wa wimbo huo, akithibitisha kuwa anatambua na kuthamini kipaji cha msanii huyo anayeinukia. Kwa kutumia ushawishi wake mkubwa katika tasnia ya muziki, Nyashinski aliipa kazi ya Toxic Lyrikali msukumo wa kipekee, hatua ambayo imeibua msisimko mkubwa miongoni mwa mashabiki wa muziki wa hip hop. Kutoka kwa mashairi hadi uwasilishaji, wimbo huo umesifiwa kwa ubora wake na kuonekana kama hatua muhimu kwa msanii huyo chipukizi. Baraka kutoka kwa Nyashinski, ambaye anatambulika kama mmoja wa magwiji wa muziki wa Kenya, imechukuliwa na mashabiki na wadau wa muziki kama ishara ya matumaini kwa kizazi kipya cha wasanii. Wengi wamepongeza moyo wake wa kuinua vipaji na kuonyesha mshikamano katika kukuza muziki wa ndani. Wimbo wa Cartman unaendelea kupata umaarufu mitandaoni huku mashabiki wakimpongeza Toxic Lyrikali kwa kazi nzuri, na kumshukuru Nyashinski kwa kuonyesha mfano wa kuigwa katika kuendeleza muziki wa Kenya kwa kushirikiana na wale wanaochipuka Wimbo wa “Cartman” wa msanii Toxic Lyrikali hadi kufikia sasa, umefikisha zaidi ya 879,000 ya watazamaji kwenye YouTube tangu kuchapishwa kwake miezi saba iliyopita.

Read More