PICHA MPYA ZA TUPAC ZAZUA GUMZO MTANDAONI
Aliyekuwa rapa kutokea Marekani, Tupac Amaru Shakur aliyefariki mwaka 1996, amezua gumzo katika mitandao mbalimbali ya kijamii baada ya picha zake kusambaa. Watu wengi wamehoji iwezekanaje picha za rapa huyo aliyefariki miaka 26 iliyopita, kuonekana na ubora zaidi kushinda hata baadhi ya picha za watu mbalimbali ambao bado wapo hai. “Picha za Tupac zina ubora kuliko picha za baadhi yetu tulio hai.” aliandika shabiki moja. “Tupac alikuwa na iphone 13 mwaka 1995?” aliuliza shabiki mwingine. Utata huo umefanya baadhi ya watu kuamini kuwa inawezekana, Tupac bado yupo hai kutokana na utata wa kifo chake, huku wengine wakimtaka rapa huyo kujitokeza kama bado yupo hai. “Tunajua bado upo hai Pac, tafadhali jitokeze tumekukumbuka sana.” aliandika shabiki mwingine.
Read More