Muonekano mpya wa Vivian wazua gumzo

Muonekano mpya wa Vivian wazua gumzo

Mwanamuziki Vivian ametuonyesha muonekano wake mpya baada ya kuzinyoa nywele zote kichwani (Kipara). Kupitia ukurasa wake wa Instagram amesema kuwa ameamua kuja na muonekano wa kitofauti kama njia ya kukumbatia ukurasa mpya wa maisha yake siku chache baada ya kuthibitisha kupitia wakati mgumu mahusiano yake na mume wake Sam West yalipoingiwa na ukungu. Muonekano wa sasa umeonekana kuteka mazungumzo zaidi mtandaoni, huku baadhi wakidai kuwa huenda mrembo huyo ana kazi mpya ambayo ataiachia hivi karibuni. Mionekano kwa wasanii si jambo la kuchukulia poa, bali ni kazi. Ni moja ya njia za branding na kujiweka machoni kwa mashabiki muda wote.

Read More
 Sam West awataka watu kutoingilia mahusiano yake na Vivian

Sam West awataka watu kutoingilia mahusiano yake na Vivian

Siku moja baada ya Sam West kuthibitisha kuwa mahusiano yake na mwimbaji Vivian yameingiwa na ukungu, sasa mchekeshaji huyo ambaye anasusua kisanaa nchini ameibuka na mpya. Kupitia mitandao ya kijamii Sam West amewataka watu kutoingilia sana sakata la ndoa yake na Vivian kuvunjika kwani huenda wakabaki njia panda ikitokea wamefufua tena penzi lao. “Methali: Mambo ya watu wawili waliopendana usiyaingilie, utaachwa katikati wakirudiana.” Ameandika Instagram. Ujumbe huo umetafsiriwa na walimwengu kuwa huenda ni kiki ya ujio mpya wa Vivian kimuziki ambapo amewataka wawili hao kuachia wimbo huo mara moja badala ya kudanganya umma kuwa jini mkata kamba ameingilia mahusiano yao. Sam West na mke wake Vivian wamekuwa gumzo mtandaoni baada ya taarifa kuibuka kuwa wawili hao wamebwaga manyanga. Utakumbuka Vivian ndiye alikuwa wa kwanza kuweka wazi kuwa anapitia wakati mgumu akitaka mashabiki wamweke kwa maombi baada ya mume wake kumkimbia licha ya kujaribu kutatua tofauti zao. Haikushia hapo Sam West pia alitumia mitandao yake kijamii kudokeza kuwa ndoa yake imefikia mwisho kwa kile alichokitaja kutoelewana kati yake na mke wake Vivian.

Read More
 Sam West athibitisha kuvunja kwa ndoa yake na Vivian

Sam West athibitisha kuvunja kwa ndoa yake na Vivian

Sam West amethibitisha kuvunjika kwa mahusiano yake na mwimbaji Vivian baada ya kudumu kwenye ndoa kwa muda wa takriban miaka sita. Kupitia ujumbe wa mafumbo aliouchapisha kwenye mtandao wa Instagram Sam West aamesema ameamua kuachana na mwimbaji huyo kwa sababu ambazo zipo nje ya uwezo wake kwani angendelea kubaki kwenye mahusiano hayo huenda angepoteza maisha yake kutokana na msongo wa mawazo. Kauli ya Sam West inakuja baada ya Vivian kuweka wazi kuwa anapitia kipindi kigumu katika maisha kufuatia mume wake kumkimbia ambapo alienda mbali zaidi na kuwataka mashabiki wamweke kwa maombi kutokana na jini mkata kamba kuingilia mahusiano yake. Hata hivyo mashabiki walitilia shaka taarifa za mrembo huyo kuachana na mume wake Sam West wengi wakihoji kuwa huenda anatafuta njia ya kuteka hisia zao kwa ajili ya ujio wa ngoma yake mpya. Utakumbuka wawili hao wamekuwa pamoja tangu mwaka wa 2016 baada ya Sam West kumvisha pete ya uchumba Vivian mubashara kwenye kipindi cha runinga ambapo mwaka wa 2018 walihalalisha mahusiano yao kwa njia ya harusi ya kitamaduni.

Read More
 VIVIAN AACHIA RASMI ALBUM YAKE MPYA

VIVIAN AACHIA RASMI ALBUM YAKE MPYA

Mwanamuziki nyota nchini Vivian ameachia rasmi album yake mpya iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki zake. Album hiyo inayokwenda kwa jina la Vivi the album ina jumla ya nyimbo 10 za moto huku ikiwa na kolabo 3 kutoka kwa wakali kama Kidum Kibido, Trio Mio na Sosuun. Album hiyo ambayo ina nyimbo kama Chachisha, good vibes, You are God,Heart of lion, na nyingine nyingi inapatikana exclusive kupitia mtandao wa kupakua na kusikiliza muziki wa Boomplay Kenya. Vivi the album ni album ya kwanza kutoka Studio kwa mtu mzima vivian tangu aanze safari yake ya muziki miaka saba iliyopita.

Read More
 SOSUUN NA VIVIAN WASHAMBULIWA MTANDAONI KWA KUTUMIA KIKI KUTANGAZA NGOMA YAO MPYA

SOSUUN NA VIVIAN WASHAMBULIWA MTANDAONI KWA KUTUMIA KIKI KUTANGAZA NGOMA YAO MPYA

Mashabiki wa muziki nchini wamewatolea uvivu wasanii Vivian pamoja na Sosuun baada wasanii hao kuonekana kutumia kiki kutangaza kazi yao mpya ambayo itaingia sokoni hivi karibuni. Kupitia mitandao yao ya kijamii wawataka Vivian na Sosuun waache suala la kuendekeza kiki kwenye muziki wao na badala yake watoe muziki mzuri ambao utajiuza wenyewe. Aidha wameenda mbali zaidi na kusema kwamba wasanii hao hawana ubunifu kwenye masuala ya kutengeneza matukio yatakayowafanya wazungumzie mtandaoni kwani kiki waliyotengeneza haina mashiko yeyote ya kuteka hisia za watu. Kauli hiyo ya wakenya mara baada ya Sosuun kurekodi video akimvamia Vivian akiwa kwenye studio za main switch na kutaka kumshushia kichapo kwa hatua ya kumvunjia heshima mapema wiki aliposema kuwa familia yake ndio imemfanya apotea kwenye game ya muziki nchini licha ya kuwa kipaji. Utakumbuka kwa sasa Vivian pamoja na Sosuun  wameachia ngoma yao mpya inayokwenda kwa jina la “Chachisha.”

Read More