Entertainment

VIVIAN AACHIA RASMI ALBUM YAKE MPYA

VIVIAN AACHIA RASMI ALBUM YAKE MPYA

Mwanamuziki nyota nchini Vivian ameachia rasmi album yake mpya iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki zake.

Album hiyo inayokwenda kwa jina la Vivi the album ina jumla ya nyimbo 10 za moto huku ikiwa na kolabo 3 kutoka kwa wakali kama Kidum Kibido, Trio Mio na Sosuun.

Album hiyo ambayo ina nyimbo kama Chachisha, good vibes, You are God,Heart of lion, na nyingine nyingi inapatikana exclusive kupitia mtandao wa kupakua na kusikiliza muziki wa Boomplay Kenya.

Vivi the album ni album ya kwanza kutoka Studio kwa mtu mzima vivian tangu aanze safari yake ya muziki miaka saba iliyopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *