VJ Patelo Amshambulia Toxic Lyrikali kwa Kuishi Maisha ya Feki

VJ Patelo Amshambulia Toxic Lyrikali kwa Kuishi Maisha ya Feki

Msanii wa Arbantone VJ Patelo ameibua upya mzozo na msanii wa hip-hop Toxic Lyrikali, akimtuhumu kuishi maisha bandia na kukosa ubunifu katika muziki wake. Kupitia ujumbe aliouchapisha kwenye mitandao ya kijamii, Patelo amedai kuwa Lyrikali hudanganya katika mashairi ya muziki kuhusu utajiri na mali anazomiliki, ikiwemo madai ya kuwa na gari la kifahari aina ya Mercedes-Benz S-Class. Amesema kuwa msanii huyo anaishi maisha ya kuigiza na kwamba madai yake kuhusu magari na pesa ni ya kutafuta umaarufu tu. Patelo pia ameongeza kuwa nyimbo nyingi za Lyrikali si za asili, akidai kwamba amekuwa akiiga nyimbo za wasanii wa Jamaica na kuzitafsiri kwa Sheng ili kuwavutia mashabiki wa muziki nchini Kenya. Amesema hakuna ubunifu wa kweli katika kazi zake, bali ni nakala za nyimbo za nje zilizotiwa ladha ya mitaani. Kauli za Patelo zimezua gumzo mitandaoni, huku mashabiki wakigawanyika kati ya wanaomuunga mkono na wale wanaomtetea Toxic Lyrikali. Hadi sasa, msanii huyo hajatoa majibu rasmi kuhusu tuhuma hizo, ingawa hii si mara ya kwanza anakosolewa kuhusu uhalisia wa nyimbo zake.

Read More
 VJ Patelo Apuuzilia Uvumi wa Kuibiwa Dandora

VJ Patelo Apuuzilia Uvumi wa Kuibiwa Dandora

Msanii kutoka Kenya VJ Patelo amekanusha vikali tetesi zilizokuwa zikisambazwa mitandaoni kwamba alivamiwa na kuibiwa Chains zake za dhahabu katika eneo la Dandora, Nairobi. Akijibu madai hayo, Patelo amesema anashangazwa na watu wanaobuni stori za uongo ili kutafuta umaarufu na kufuata vichwa vya habari. Ametoa msimamo wake kwamba hajawahi kuibiwa wala kushambuliwa Dandora, na kwamba ukimya wake mtandaoni ni wa kawaida kutokana na ratiba zake binafsi. Aidha, amewataka wafuasi wake kupuuza taarifa zisizo na msingi na kuendelea kumuunga mkono katika kazi zake za sanaa. Uvumi huo ulianza baada ya jamaa mmoja kudai kuwa Patelo alinyang’anywa mali zake, jambo ambalo limepelekea mashabiki wengi kuhoji ni kwa nini hakuwa akiposti kwenye mitandao ya kijamii kwa siku mbili zilizopita.

Read More
 VJ Patello Amchana Diana B Baada ya Madai ya Chain Feki

VJ Patello Amchana Diana B Baada ya Madai ya Chain Feki

Mzozo kati ya VJ Patello na Influencer aligeukia muziki Diana B umeendelea kuchukua sura mpya baada ya Patello kujibu vikali madai ya kwamba mikufu yake ya dhahabu ni bandia. Kupitia Instagram, Patello alimshutumu Diana na mumewe Bahati kwa kushindwa kulipa shilingi milioni moja kwa Harambee Stars, akiongeza kuwa wawili hao hawana uhalali wa kuzungumzia vitu vya thamani. Ugomvi huo ulianza baada ya Patello kukosoa wimbo mpya wa Diana B uitwao Bibi ya Tajiri, ambapo Diana alisikika akijinadi kuwa ndiye rapa bora nchini Kenya huku akionekana kwenye video akirarua picha za marapa maarufu kama Khaligraph Jones na Nyashinski. Kitendo hicho kilimkera Patello ambaye alimtolea uvivu kwa kudai kuwa hana heshima kwa wasanii halisi wa hiphop, akamtaka aendelee na masuala ya content creation kwa sababu hajui kurap. Diana B hakusita kujibu mashambulizi hayo kwa kumdharau Patello, akisema kwa kejeli kwamba ni ajabu mtu mwenye mikufu bandia anathubutu kukosoa kazi ya “Bibi ya Tajiri”

Read More
 DJ Shiti Asababisha Vicheko kwa Video ya Maombi ya Sheng kwa Patelo

DJ Shiti Asababisha Vicheko kwa Video ya Maombi ya Sheng kwa Patelo

Mchekeshaji maarufu DJ Shiti ameibua kicheko mitandaoni baada ya kujitokeza kwa njia ya ucheshi kumuombea VJ Patelo, kufuatia tetesi kwamba ndoa yake na mkewe Dee imeingiwa na ukungu. Kupitia video ambayo kwa sasa inasambaa, DJ Shiti amesikika akitumia lugha tata ya Sheng kuomba mikosi imuondokee Patelo. Lugha hiyo, iliyojaa maneno ya ucheshi na misemo isiyoeleweka kirahisi, imewafanya mashabiki wengi kucheka huku wengine wakisema maombi hayo ndiyo dawa ya jini mkata kamba linalodaiwa kuingia kwenye ndoa ya Patelo. “Baba nakabidhi Patelo mikono mwako, chude ngenje, chude ngenje siku zombotote ngezo zikuje nyingi. Ngezo zikuje kama zombotote apate shagla kama zombotote. Nakataa maroho ya chang’ili nakataa roho ya black devil. Nambariki na roho ya Captain Morgan siku zombotote. Gota hatujawahi bugunda!!”, Alisikika akisema kwenye video inayosambaa mtandaoni. Video ya DJ Shiti imekuja siku chache baada ya ile iliyosambaa ikimuonyesha Dee akimzaba kofi Patelo walipokuwa katika nightclub moja jijini Nairobi, tukio lililoibua tetesi kwamba ndoa yao inakumbwa na changamoto. Hata hivyo, VJ Patelo mwenyewe amekanusha vikali madai hayo, akisisitiza kuwa ndoa yake iko imara na haina misukosuko. Akiwa amekasirishwa na tetesi hizo, Patelo aliwaambia wakosoaji wake wajishughulishe na maisha yao badala ya kufuatilia mambo ya kifamilia yake. Kauli ya Patelo imeonekana kama onyo kali kwa wanaoendeleza uvumi mitandaoni, huku DJ Shiti akigeuza sakata hilo kuwa kichekesho kwa maombi yake ya Sheng ambayo yamewachekesha wengi.

Read More