WhatsApp Yazindua Kipengele Kipya cha Ku-forward Status kwa Marafiki
Kampuni ya Meta, inayomiliki jukwaa maarufu la mawasiliano la WhatsApp, imeanza kutekeleza kipengele kipya kinachoruhusu watumiaji ku-forward Status kwa marafiki au kwenye Status zao wenyewe. Hili ni moja ya maboresho makubwa katika eneo la Status, linalokusudia kuongeza mwingiliano na urahisi wa kushirikiana maudhui kati ya watumiaji. Kwa kutumia kipengele hiki, mtumiaji anaweza kuchagua Status ya mtu mwingine iwe ni picha, video au maandishi na kuishiriki (forward) moja kwa moja kwa mtu mwingine au kuipost kwenye Status yake binafsi. Hii ni hatua inayofanana na mtindo wa kushirikiana Stories kwenye majukwaa mengine kama Instagram na Facebook. Mbali na kuongeza urahisi wa kushirikisha maudhui, WhatsApp pia imetoa chaguo la faragha, ambapo watumiaji wanaweza kuchagua kama wanataka status zao ziweze kushirikiwa na wengine au la. Hii inawapa watumiaji udhibiti kamili wa maudhui yao na jinsi yanavyosambazwa. Kipengele hiki kimeanza kusambazwa kwa baadhi ya watumiaji kupitia masasisho ya hivi karibuni, na kinatarajiwa kupatikana kwa wote katika siku zijazo. Watumiaji wa Android na iOS wanashauriwa kuhakikisha wanatumia toleo la kisasa la WhatsApp ili kufurahia huduma hii mpya.
Read More