WHATS APP KWENYE MAJARIBIO MAPYA, KULETA URAHISI KWA MA-ADMIN

WHATS APP KWENYE MAJARIBIO MAPYA, KULETA URAHISI KWA MA-ADMIN

App maarufu ya mtandao wa kijamii ya WhatsApp ipo kwenye kufanya majaribio ya kuweka sehemu mpya ya WhatsApp Communities. Inaelezwa kuwa, sehemu ya Communities itakuwa ni maalum kwa viongozi wa vikundi (Group Admins) kuona group zote ambazo wanazisimamia. Inatajwa kuwa ni sehemu ya kusimamia groups zote ambazo Admins anazisimamia na atakuwa na uwezo wa kutuma message katika groups nyingi kwa pamoja.

Read More
 WHATSAPP MBIONI KUWEKA MFUMO WA REACTIONS KATIKA CHATS ZA WATUMIAJI WAKE

WHATSAPP MBIONI KUWEKA MFUMO WA REACTIONS KATIKA CHATS ZA WATUMIAJI WAKE

Kwa muda mrefu WhatsApp imeendelea kufanya majaribio ya kuweka mfumo wa Reactions katika chats. Reactions ni mfumo wa kuonyesha hisia au response yako katika message, unaweza kuonyesha kupendezwa, kushangaa, kucheka au kupinga jambo kwa kuchagua emoji inayoendana na mtazamo wako. Feature hii ipo katika Facebook na Instagram lakini katika platform hizo unaweza kuchagua emoji yoyote. Hivi karibuni WhatsApp imekuwa ikijaribu mfumo wa reactions katika app yake ya PC. Imeanza na app ya Mac na soon itaanza majaribio kwa watumiaji wa Windows. Inaonekana WhatsApp inakamilisha majaribio katika platform zote kabla ya kuachia mabadiliko hayo kwa watumiaji wote.

Read More
 WHATSAPP MBIONI KUJA NA UWEZO WA KUENDELEA KUSIKILIZA VOICE MESSAGES HATA UKIWA UMEFUNGA CHATS

WHATSAPP MBIONI KUJA NA UWEZO WA KUENDELEA KUSIKILIZA VOICE MESSAGES HATA UKIWA UMEFUNGA CHATS

App ya WhatsApp inafanya majaribio ya kuweka mfumo mpya wa “Voice Message au Notes”. Mfumo huo mpya utawezesha watumiaji kuendelea kusikiliza Voice Message hata ukiwa umefunga chat na kufungua chat nyingine au kurudi kwenye list ya messages.   Kwa kawaida ukiwa unasikiliza Voice Message katika WhatsApp, ukiifunga chat na Voice Message inaacha kucheza, hivyo inabidi ubaki katika chat ikiwa unataka kusikiliza Voice Message. Mfumo mpya wa Voice Messages utawezesha mtumiaji kuendelea kusikiliza Voice Message huku akiwa amefungua chat nyingine tofauti na chat ambayo Voice Message imetumwa.   Kwa juu itakwepo line ya rangi ambayo inafanana na Audio Player ambapo mtumiaji atakuwa na uwezo wa ku-pause, Play na kufunga Voice Message. Lakini pia  voice note hiyo itakuwa na uwezo wa kuonyesha jina na profile ya chat ambayo imetuma Voice Message.  Itasaidia endapo kama kuna chats nyingine ambazo inakubidi ufungue kwani utakuwa na uwezo wa kuendelea na shughuli nyingine katika app hiyo huku ukisikiliza Voice Message kwa pamoja.   Feature hii ipo katika majaribio katika mfumo wa iOS, na itatoka kabla ya mwaka huu kuisha. Ni mabadiliko ambayo tayari yapo Telegram kwa muda mrefu sana.            

Read More