Mwimbaji William Getumbe akanusha kutumia suala la kukojoa kitandani kutafuta kiki

Mwimbaji William Getumbe akanusha kutumia suala la kukojoa kitandani kutafuta kiki

Mwanamuziki wa injili kutoka Eldoret William Getumbe amefunguka kwa mara ya kwanza juu ya kutumia suala la kukojoa kitandani kutafuta kiki. Kwenye mahojiano na Nicholas Kioko, Getumbe amekanusha madai ya kutumia hali yake kutengeneza mazingira ya kuzungumziwa mtandaoni huku akisema kuwa aliamua kuweka wazi masaibu yake kwa umma kwa ajili ya kuondoa mitazamo hasi kwa watu wanaokojoa kitandani. Bosi huyo wa Billgates Records amesema amekuwa akikumbana na tatizo hilo kwa kipindi cha miaka minne sasa, jambo ambalo limempelekea kuvalia nepi kama njia ya kuepuka aibu katika jamii. Hata hivyo Getumbe mwenye umri wa miaka 48 amewataka wanaume wanaopitia hali kama yake kutojificha na badala yake wawashirikishe wake zao ili kuzuia migogoro kwenye ndoa. Kauli yake imekuja mara baada ya kukiri kwenye mahojiano na Tuko kwamba amekuwa akikojoa kitandani akiwa kwenye ndoa ambapo alienda mali zaidi na kusema kuwa mke wake Virginia Masitha, amekuwa akimvisha nepi nyakati za usiku, kumuepusha kulowesha malazi yao kwa mkojo.

Read More
 Mwanamuziki William Getumbe akiri kuteswa na tatizo la kukojoa kitandani

Mwanamuziki William Getumbe akiri kuteswa na tatizo la kukojoa kitandani

Mwimbaji wa nyimbo za injili kutoka Eldoret, William Getumbe, amefunguka kuhusu maisha yake ya ndani kwa kukiri kuwa ana tatizo la kukojoa kitandani nyakati za usiku. Kwenye mahojiano na Tuko Getumbe amefichua kuwa mke wake Virginia Masitha, amekubali hali yake hiyo na amekuwa akimvisha nepi kabla ya kulala usiku, jambo ambalo amedai kuwa umuepusha kulowesha malazi yao kwa mkojo. Msanii huyo wa kibao cha Fuata Yesu amesema watu wengi wazima ambao ukojoa kitandani huwa hawapendi kuwashirikisha wapenzi wao, jambo amedai limevunja ndoa ya familia nyingi. Hata hivyo amewashauri watu wenye tatizo hilo kukubali hali zao na badala yake kutumia nepi kama njia ya kuepuka aibu. Kukojoa kitandani ni hali inayotokea ambapo mkojo hutoka wenyewe usiku wakati wa kulala na ni ishara ya matatizo ya udhibiti wa kibofu cha mkojo kama ya kushindwa kujizuia kukojoa (incontinence) au kibofu cha mkojo kufanya kazi kuliko kawaida. Utafiti unaonyesha kwamba asilimia 1 hadi 2 ya watu wazima hukojoa kitandani, ingawa watafiti wamaamini kwamba takwimu hizi ni za chini kutokana na kwamba watu hawajitokezi kwa sababu ya kuona aibu.

Read More