WINNIE NWAGI MASHAKANI KWA KUKWEPA DENI LA SHILLINGI ELFU 9 ZA KENYA

WINNIE NWAGI MASHAKANI KWA KUKWEPA DENI LA SHILLINGI ELFU 9 ZA KENYA

Msanii kutoka Uganda Winnie Nwagi ameingia kwenye headlines mara ya kudaiwa kukwepa kulipa deni la shillingi elfu tisa analodaiwa na night club moja nchini humo. Kulingana na vyanzo vya karibu na night club hiyo, Nwagi amekuwa akila chakula pamoja na kuagiza vinywaji kwa kipindi cha miezi mitatu bila malipo yeyote. Chanzo hicho kimeenda mbali na kudai baada ya uongozi night club hiyo kumtaka alipie gharama ya huduma aliyopewa, alihamua kuingia na jeuri kiasi cha kumtishia maisha mmiliki wa eneo hilo la burudani. Hata hivyo ni jambo ambalo lilipelekea uongozi wa night club hiyo kukata mshahara wa mfanyikazi aliyemhudumia Winnie Nwagi kwa ajili ya kukamilisha deni hilo.

Read More
 WINNIE NWAGI AFUNGUKA TUHUMA ZA KUKATAA KULIPA KIINGILIO KWENYE MOJA YA NIGHT CLUB

WINNIE NWAGI AFUNGUKA TUHUMA ZA KUKATAA KULIPA KIINGILIO KWENYE MOJA YA NIGHT CLUB

Mwanamuziki kutoka Uganda Winnie Nwagi amejibu tuhuma za walinzi kumzuia kuingia kwenye moja ya klabu ya usiku huko Kololo nchini Uganda baada ya kususia kulipa kiingilio. Kwenye video aliyoposti Snapchat Nwagi mrembo huyo amekiri kuzozana na walinzi wa club hiyo kwa kusema kuwa alishangazwa na hatua yao kumtaka alipe kiingilio wakati nyimbo zake zimekuwa zikipigwa kwenye eneo hilo la burudani. Hitmaker huyo wa “Malaika” amesisitiza kuwa wasanii wanapaswa kupewa heshimu kwa kazi zao za muziki badala ya kukandamizwa. Kauli ya Winnie Nwagi imekuja mara baada ya chanzo kimoja kukiambia jarida moja la habari nchini Uganda kuwa msanii huyo pamoja na marafiki zake watano walizuiliwa kuingia kwenye club moja ya usiku kwa madai ya kukataa kulipa kiingilio. Chanzo hicho kilienda mbali zaidi na kumtaka Winnie Nwagi aheshimu biashara za watu licha ya kuwa mtu maarufu.

Read More
 WINNIE NWAGI AKIRI KUINGIA NA HOFU KWA KUKOSA WAFADHILI WA SHOW YAKE

WINNIE NWAGI AKIRI KUINGIA NA HOFU KWA KUKOSA WAFADHILI WA SHOW YAKE

Mwanamuziki Winnie Nwagi ameshinndwa kuficha furaha yake mara baada ya kuwapata wafadhili wa tamasha lake la muziki linalotarajiwa kufanyika Septemba 9 katika ukumbi wa Oval Criket huko Lugogo viungani mwa jiji la Kampala. Kwenye mkao na waandishi wa habari, Winnie Nwagi amesema aliingiwa na hofu baada ya wafadhili kushindwa kujitokeza alipotangaza ujio wa tamasha lake hilo. “Niliogopa sana. Unajua gharama zinaweza kuwa kubwa lakini nilijua nitapata wadhamini wazuri na namshukuru Mungu nilipata.” Nwagi hadi sasa ameukaribisha udhamini wa chapa ya bia, iitwayo Club beer, na vituo vya redio nchini Uganda licha ya kushindwa kupata wafadhili ndani ya kipindi cha mwezi mmoja alipotoa tangazo kuhusu tamasha lake la muziki.

Read More
 WINNIE NWAGI AJITAPA KUFANYA TAMASHA LAKE BILA MATANGAZO KWENYE VYOMBO VYA HABARI

WINNIE NWAGI AJITAPA KUFANYA TAMASHA LAKE BILA MATANGAZO KWENYE VYOMBO VYA HABARI

Msanii wa Swangz Avenue Winnie Nwagi juzi kati alitangaza kufanya tamasha lake la muziki Septemba 9 mwaka huu huko Cricket Oval Lugogo viungani mwa jiji la Kampala. Hii ni baada ya Swangz Avenue kuitikia mwito wa mashabiki ambao walikuwa wanaipa shinikizo lebo hiyo kuandaa tamasha la msanii huyo kutokana na wao kuonekana kuwapendelea wasanii Vinka pamoja na Azawi. Licha ya kwamba Winnie Nwagi hanaitaji vyombo vya habari kutangaza tamasha lake lijalo liwafikie wengi mrembo huyo amejitokeza na kujinadi kuwa haitaji usaidizi wa mtu yeyote ndio aweze kujaza ukumbi wa Cricket oval kwani ana uwezo wa kufanya hivyo mwenyewe kutokana na alama ambayo ameiacha kwenye tasnia ya muziki kwenye tasnia ya muziki nchini Uganda. “I don’t need you to advertise for me. I can pull it off without publicity,” Winnie Nwagi amejibu shabiki kwenye mtandao wa twitter ambaye alichapisha ujumbe kuhusu onesho lake la muziki. Kwa miaka kadhaa sasa winnie nwagi amegonga vichwa vya habari kutokana matukio yake ya kushangaza ikiwemo kumshushia kichapo mfanyikazi wake wa nyumbani, kuvalia mavazi yanaonyesha uchi wake, na kuwatusi wakosoaji wake kwenye mitandao ya kijamii. Tunaamini miendo yake isiyoridhisha haitafanya mashabiki kutohudhuria tamasha lake la muziki.

Read More
 PROMOTA WA LONDON ATISHIA KUICHUKULIA HATUA KALI LEBO YA SWANGZ AVENUE

PROMOTA WA LONDON ATISHIA KUICHUKULIA HATUA KALI LEBO YA SWANGZ AVENUE

Promota wa Uganda wanayoishi mjini London Maama Africa ametishia kuhakikisha kuwa waimbaji wote wa Swangz Avenue wamepigwa marufuku kusafiri hadi London, lebo hiyo isipomlipa fidia ya euro 65000. Promota hao anadai kuwa alilipa Euro 5000 ili Winnie Nwagi atumbuize London lakini siku ya tukio, Nwagi pamoja na Fik Fameika walikataa kutoa burudani kwa mashabiki hadi usiku wa manane wakati walipotumbuiza nyimbo chache. Lakini pia wasanii hao walivunja mkataba na kutumbuiza kwenye shoo nyingine iliyopewa jina la “Chill and Grill” kwa kutumia kibali chake cha kazi, kitu ambacho anaona si cha kingwana. “Nataka kuwafundisha uweledi waimbaji wa Uganda. Nililipa na kugharamia kila kitu kwa Winnie Nwagi, lakini alienda mbali zaidi na kutumbuiza katika hafla nyingine bila idhini yangu,” alisema katika mahojiano na MwanaYouTube. Promota hao wameongeza, “Aliimba nyimbo chache tu baada ya kuchelewa kufika. Nimeiandikia Swangz avenue kuhusu kitendo hicho na ninatarajia jibu kabla ya Jumatatu la sivyo nitahakikisha kuwa wasanii wake wanapigwa marufuku kutumbuiza London.” Hata hivyo Maama Africa wanahusisha kuporomoka kwa onyesho hilo na vitendo visivyo vya kitaaluma vya Winnie Nwagi.

Read More
 WINNIE NWAGI AAPA KUTOFANYA KAZI NA WASANII WA NIGERIA

WINNIE NWAGI AAPA KUTOFANYA KAZI NA WASANII WA NIGERIA

Staa wa muziki kutoka Uganda Winnie Nwagi amefunguka kuhusu kufanya kazi na wasanii wa Nigeria. Katika mahojiano yake hivi karibuni Nwagi amesema hatokuja kufanya muziki na wasanii wa nigeria kwa kuwa wanapenda sana kuwatumia wasanii wa mataifa mengine kujitafutia makuu. Msanii huyo wa Swangz Avenue amesema wanigeria wamekuwa na mazoea ya kuwatumia wasanii wengi vibaya kusukuma brand au chapa yao ya muziki  katika soko la uganda lakini nchini kwao hawatangazi kazi za waganda. Utakumbuka Winnie Nwagi amewahi kufanya kazi na mwanamuziki kutoka Nigeria Slim Prince kupitia ngoma yao inayokwenda kwa jina la Fire Dance.

Read More
 WINIE NWAGI AKIRI KUPATA MSONGO WA MAWAZO KISA MASHABIKI

WINIE NWAGI AKIRI KUPATA MSONGO WA MAWAZO KISA MASHABIKI

Winnie Nwagi ni moja kati ya wasanii nchini Uganda wasiotaka masihara  kutokana kwa mashabiki wanaomkosoa kwenye  mitandaoni ya kijamii. Katika mahojiano yake hivi karibuni Winnie Nwagi amefichua kwamba alipatwa na msongo wa mawazo kutokana na matusi ya mashabiki mtandaoni. Hitmaker huyo wa malaika amesema alikuwa analia kila mara anaposoma comment za mashabiki wanaotukana kwenye mitandao ya kijamii lakini alilazimika kupambana wanaomkatisha tamaa mtandaoni kwa kuwa block wanaomuandikia jumbe za matusi dhidi yake.

Read More
 WINNIE NWAGI AFUNGUKA KUHUSU MADAI YA KUTENGWA NA SWANGZ AVENUE

WINNIE NWAGI AFUNGUKA KUHUSU MADAI YA KUTENGWA NA SWANGZ AVENUE

Msanii wa Swangz Avenue Winnie Nwagi amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu tetesi za lebo hiyo kumpendelea msanii mwenzake Azawi huku wakimtenga. Katika mahojiano yake hivi karibuni Winnie Nwagi amewatolea hofu mashabiki zake kwa kusema kuwa yupo mbioni kuja na onesho lake ambalo ana imani kuwa itapata mapokezi makubwa. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Malaika” amesema hana la kusema kuhusu tamasha la Azawi linalotarajiwa kufanyika hivi karibuni kwa sababu kila mtu katika maisha ana bahati na muda wake. Kauli ya Winnie nwagi imekuja mara baada ya mashabiki kuisuta vikali lebo ya swangz avenue kwa hatua ya kumuandalia onesho la muziki msanii Azawihuku wakimuacha pembeni winnie nwagi ambaye amekuwa chini ya lebo hiyo kwa muda mrefu.

Read More
 WINNIE NWAGI AZUA GUMZO MTANDAONI BAADA YA KUMSHUSHIA KICHAPO SHABIKI KWENYE MOJA YA PERFORMANCE

WINNIE NWAGI AZUA GUMZO MTANDAONI BAADA YA KUMSHUSHIA KICHAPO SHABIKI KWENYE MOJA YA PERFORMANCE

Winnie Nwagi ni moja kati ya wasanii ambao watu wengi nchini Uganda wanamtaja kama malkia wa kashfa nchini humo kutokana vituko vyake. Wikiendi hii iliyopita kwenye moja ya performance yake alimsaba makofi shabiki yake mmoja ambaye alijaribu kumchukua video akiwa jukwaani bila ridhaa yake. Kwenye moja ya video inayosambaa mitandaoni Winnie Nwagi anaoneka akimshushia kichapo cha mbwa shabiki yake huyo kwa kumsaba makofi matatu ya moto. Kutokana na hilo walimwengu kwenye mitandao ya kijamii wameonekana kutofurahishwa na kitendo hicho ambapo wamemtaka winnie nwagi akome kuwashambulia mashabiki ambao ukoshwa na mtindo wa mavazi yake ambayo mara nyingi uonesha maungo yake ya mwili kwa umma. Hata hivyo baadhi ya mashabiki wametishia kususia matamasha yake ya muziki iwapo ataendelea na kasumba hiyo ya kuwavamia mashabiki wanaomuunga mkono kwenye muziki wake.

Read More
 MWANAMUZIKI WA SWANGZ AVENUE WINNIE NWAGI AWATOLEA UVIVU MASHABIKI WAKE WA DUBAI

MWANAMUZIKI WA SWANGZ AVENUE WINNIE NWAGI AWATOLEA UVIVU MASHABIKI WAKE WA DUBAI

Mwanamuziki Winnie Nwagi ni moja kati ya watu ambao wanazungumza kilicho akilini mwao bila kushurutishwa na mtu yeyote. Lakini pia huwa anawajibu wakosoaji wake bila uwoga wotewote. Hitmaker huyo wa ngoma ya Kwata Essimu amewatolea uvivu mashabiki zake wa Dubai ambao juzi kati walimshambulia baada ya kudinda kupiga nao picha. Kulingana na mashabiki hao, Winnie Nwagi alikataa kupiga nao picha baada ya kusafiri mwendo mrefu kwenda kumuona hotelini. Sasa kupitia video aliyoichapisha kwenye mitandao yake ya kijamii winnie nwagi amesema ana haki ya kutopiga picha na mashabiki hivyo mashabiki wanapaswa kujifunza kuwaheshimu wasanii. Mrembo huyo ameenda mbali zaidi na kusema kuwa hajutii kitendo cha kukataa kupiga picha na mashabiki huku akiwataka wanaomkosoa kwa hatua yake hiyo washughulike na maisha yao. “Simuogopi mtu yeyote isipokuwa Mungu, Hauna sababu ya kushurutisha kupiga picha nami,” alisikika kwenye audio clip inayosambaa mitandaoni. Utakumbuka Winnie Nwagi amekuwa akikosolewa kila mara na mashabiki wa muziki nchini Uganda kutokana na mienendo yake inayokwenda kinyume na maadili ya jamii

Read More
 WINNIE NWAGI AWACHANA WAKOSOAJI WA MAVAZI YAKE KWENYE MITANDAO YA KIJAMII

WINNIE NWAGI AWACHANA WAKOSOAJI WA MAVAZI YAKE KWENYE MITANDAO YA KIJAMII

Msanii wa Swangz Avenue Winnie Nwagi amemtolea uvivu wanaokosoa uvaaji wake wa mavazi kwenye mitandao ya kijamii. Akipiga stori na runinga moja nchini Uganda Winnie Nwagi amewataka wanaochukia mtindo wake wa mavazi wampe kazi ya kumuingizia kipato ili avae mavazi wanazozipenda. Hitmaker huyo wa “Kwata Essimu” amesema hayupo dunia kumfurahisha mtu yeyote ila yupo kwa ajili ya kumfanya binti yake awe mwenye furaha zaidi ambapo amewataka wanaomtusi kwenye mitandao ya kijamii wajipe shughuli zitakazowaingizia hela badala ya kufuatilia maisha yake. Itakumbukwa Winnie Nwagi amekuwa gumzo nchini Uganda kutokana na mtindo wake wa mavazi yanayokwenda kinyume na maadili ya jamii.

Read More
 WINNIE NWAGI MBIONI KUACHA MUZIKI

WINNIE NWAGI MBIONI KUACHA MUZIKI

Inaonekana msanii wa Swangz Avenue Winnie Nwagi hana furaha kwa sasa kwenye tasnia ya muziki nchini Uganda. Kulingana na posts zake kwenye mitandao ya kijamii hitmaker huyo wa “Musawo” inaonekana anapitia kipindi kigumu kwenye maisha yake ambayo hajawahi kutana nayo tangu aanze safari yake ya muziki. Kupitia ukurasa wake wa twitter mrembo huyo amesema kwamba kama angekuwa na kitu kingine cha kufanya kwenye maisha, angeacha muziki kabisa. Winnie nwagi amesema amechoshwa na kile kinachoendelea kwenye maisha yake kwa sasa a ameomba dua kwa mwenyezi mungu aingilia maisha yake kabla hajachukua maamuzi magumu. Kuthibitisha kwamba Winnie Nwagi hana furaha kabisa alienda mbali zaidi na kuwablock mashabiki wake wote kwenye mtandao wa instagram wasiweze ku comment kwenye post yake. Hata hivyo mrembo huyo hajaweka wazi kinachomsumbua kwa sasa kwenye maisha yake.

Read More