Wizkid Aghairi Baadhi Matamasha Kufuatia Mauzo Duni ya Tiketi

Wizkid Aghairi Baadhi Matamasha Kufuatia Mauzo Duni ya Tiketi

Msanii nyota wa muziki wa Afrobeats, Ayodeji Balogun almaarufu kama Wizkid, ameripotiwa kughairi baadhi ya matamasha yake yaliyopangwa kufanyika katika kumbi mbalimbali barani Ulaya na Marekani, baada ya kukumbwa na changamoto ya mauzo duni ya tiketi. Kwa mujibu wa vyanzo vya karibu na waandaaji wa ziara hiyo, baadhi ya miji haikufikia viwango vya mauzo yaliyotarajiwa, hali iliyowalazimu waandaaji kufuta au kuahirisha baadhi ya tarehe zilizokuwa kwenye ratiba. Hata hivyo, wachambuzi wa tasnia ya burudani wanasema hali hii haipaswi kuchukuliwa kama dalili ya kuporomoka kwa kazi ya msanii huyo ambaye amewahi kushinda tuzo nyingi za kimataifa. “Changamoto ya mauzo ya tiketi inawakumba wasanii wengi kwa sasa, si Wizkid pekee. Hata Beyoncé alikumbwa na hali kama hii katika baadhi ya maeneo kwenye ziara yake ya hivi karibuni,” alisema mchambuzi wa burudani, Doreen Obasi. Kulingana na wachambuzi hao, kushuka kwa mauzo ya tiketi kunachangiwa na sababu mbalimbali, ikiwemo hali ya kiuchumi duniani, gharama ya juu ya maisha, pamoja na ushindani mkubwa katika ratiba ya burudani ya kimataifa. Licha ya hali hiyo, muziki wa Wizkid bado unaendelea kufanya vizuri kwenye majukwaa ya kidijitali kama Spotify na Apple Music, huku nyimbo zake zikisalia maarufu katika nchi nyingi za Afrika na diaspora. “Hatuwezi kupima mafanikio ya msanii kwa kigezo cha tiketi pekee. Wizkid bado ana ushawishi mkubwa katika muziki wa kimataifa,” aliongeza Obasi. Mashabiki wake wameshauriwa kutobadili mtazamo wao dhidi ya msanii huyo, kwani hali ya sasa inaweza kuwa ya muda tu, na tayari kuna juhudi zinafanywa kurekebisha mikakati ya usambazaji na utangazaji wa matamasha yajayo. Kwa sasa, Wizkid bado anatarajiwa kutumbuiza katika baadhi ya miji mikuu duniani ambako mauzo ya tiketi yamekuwa ya kuridhisha, huku akijipanga upya kwa msimu mpya wa burudani.

Read More
 Wizkid atangaza kufanya tamasha kubwa la muziki, London Uingereza

Wizkid atangaza kufanya tamasha kubwa la muziki, London Uingereza

Msanii wa Nigeria Wizkid rasmi ametangaza onesho lake ambalo litafanyika katika uwanja wa Klabu ya Tottenham Hotspur, Jijini London Uingereza. Kwenye tangazo hilo ambalo limeiteka mitandao yote duniani kwa sasa, Mshereheshaji wa Klabu ya Tottenham, aliingia Twitter na kuweka video ikimuonesha aki-vibe na wimbo wa Wizkid ndani ya uwanja huo. Uwanja huo unabeba watu 62,850 katika matukio ya mpira lakini unabeba jumla ya watu 100,000 kwenye matamasha ya Muziki. Bado tarehe rasmi ya onesho hilo haijatangazwa lakini tiketi tayari zimeanza kuuzwa mtandaoni.

Read More
 Wizkid aomba radhi mashabiki kwa kususia show

Wizkid aomba radhi mashabiki kwa kususia show

Staa wa muziki nchini Nigeria Wizkid ameomba msamaha mashabiki zake wa Ghana kwa kushindwa kutokea kwenye show yake mjini Accra nchini Ghana siku ya Jumamosi licha kutua nchini humo. Kupitia kurasa zake za mitandao ya Kijamii amesema kwamba kuna mambo hayakuwa sawa hasa upande wa kiufundi na usalama wake. Pia ameongeza kwamba, muda wowote atatangaza tarehe mpya ya kufanya show hiyo. Katika hatua nyingine mkali huyo pia hakutokea kwenye show yake aliyokuwa aifanye jana Jumapili huko Abidjan nchini Ivory Coast, na inatajwa kuwa alikuwa tayari ametua nchini humo ila kwenye show hakutokea. Tukio hili bado halijatolewa ufafanuzi na uongozi wa mkali huyo, ila taarifa iliyopo hadi sasa, uongozi wake unashikiliwa na Polisi mjini Abidjan.

Read More
 Wizkid aingiza zaidi ya Ksh Millioni 122 kwenye onesho lake la Madison Square Garden

Wizkid aingiza zaidi ya Ksh Millioni 122 kwenye onesho lake la Madison Square Garden

Staa wa muziki nchini Nigeria Wizkid ametajwa kuingiza ($1 million) zaidi ya kSh. milioni 122 kwenye onesho lake lililofanyika katika ukumbi wa Madison Square Garden Jijini New York, November 16 mwaka huu. Hii inaingia kwenye rekodi ya kuwa onesho lake lililoingiza mkwanja mrefu zaidi kwa muda wote. Onesho hilo ambalo ni sehemu ya ziara yake ya “More Love, Less Ego” liliuza Jumla ya Tiketi 12,901 sawa na asilimia 100. Bei ya chini ya Tiketi ilikuwa ni ($77.72) sawa na kSh. 9,536 huku bei ya juu ikiwa ni ($997) takribani kSh. millioni122,331

Read More
 Wizkid awaponda wanamuziki wa Hiphop Afrika

Wizkid awaponda wanamuziki wa Hiphop Afrika

Hitmaker wa “Essence”, Msanii Wizkid ameviteka vichwa vya habari vya mitandao yote ya burudani, hii ni kufuatia kauli yake kwamba Muziki wa Hip Hop umekufa. Kwenye mahojiano na 10 Magazine, Wizkid amekaririwa akisifia ukuaji wa muziki wa Afrobeats Kimataifa huku akiuponda Muziki wa Rap. Mwanamuziki huyo kutoka Nigeria amesema mbali na Afrobeats, huwa hasikilizi aina nyingine ya Muziki hasa Rap kwa sababu nyimbo nyingi zinazotengenezwa zinaboa. Hata hivyo hakuishia hapo, aliendelea na mashambulizi yake juu ya Hip Hop ambapo alihamia kwenye mtandao wa Snapchat na kuwatolea uvivu wasanii wa Rap Afrika kwa kusema, kando na Nasty C, Sarkodie na Black Sherif wengine wote ni hovyo na ni watu waliofulia kisanaa.

Read More
 Wizkid kuachia Album mpya mwakani

Wizkid kuachia Album mpya mwakani

Staa wa muziki kutoka Nigeria Wizkid anaendelea kutupasha kuhusu album yake mpya ijayo aliyoipa jina la “SeiLess”. Kupitia insta story yake ameeleza itaachiwa kati ya mwaka huu 2022 au mwanzoni mwa 2023. Ikumbukwe, “SeiLess” inaenda kuwa album ya SITA ya Wizkid baada ya “More Love, Less Ego” ambayo imetoka wiki mbili zilizopita ikiwa ni album ya TANO. Album zingine za WizKid ni Superstar (2011), Ayo (2014), Sounds from the Other Side (2017) na Made in Lagos (2020).

Read More
 Wizkid amu-unfollow Tems kwenye mtandao wa Instagram

Wizkid amu-unfollow Tems kwenye mtandao wa Instagram

Mwanamuziki kutoka nchini Nigeria Wizkid amu-unfollow msanii mwenzake Tems kwenye mtandao wa Instagram. Wawili hao ambao wmefanikiwa kutengeneza Hit Song ya Dunia “Essence” wameonekana kuwa mbalimbali kwa muda jambo ambalo mashabiki walianza kujiuliza maswali juu ya mahusiano yao. Hatua hiyo ya Wizkid kumpunguza Tems kwenye orodha ya wafuasi wake kwenye mtandao wa instagram imekuja ikiwa ni wiki chache toka Wizkid aachie kolabo yake na Ayra Star “SUGAR” Pamoja na Wikzid kumpunguza Tems lakini bado Tems ame mfollow Wizkid kwenye mtandao huo wa instagram

Read More
 Album mpya ya Wizkid kutoka Novemba 14 mwaka huu

Album mpya ya Wizkid kutoka Novemba 14 mwaka huu

Ni rasmi sasa, tarehe mpya ya kuachiwa kwa album ya Wizkid imetangazwa, mkali huyo ataachia album yake mpya “More Love Less Ego” Novemba 14. Album hiyo ya Wizkid ilikuwa imepangwa itoke Ijumaa ya wiki hii lakini kufuatia msiba wa mtoto wa kiume wa mwanamuziki mwenzake Davido, Ifeanyi Adeleke (3) ambaye amefariki mapema wiki hii, Wizkid akaghairisha kutoa album hiyo. Na kudhihirisha umma kwamba hakuna uhasama kati yake na Davido, yeye pia ameguswa na msiba huo. Album hii mpya ya Wizkid inaenda kuwa album yake ya tano baada ya “Made In Lagos” ambayo ni ya nne, ilitoka Oktoba 30, mwaka 2020.

Read More
 BURNA BOY AWATOLEA UVIVU MASHABIKI WA WIZKID KISA KUPONDA MAFANIKIO YA ALBUM YAKE

BURNA BOY AWATOLEA UVIVU MASHABIKI WA WIZKID KISA KUPONDA MAFANIKIO YA ALBUM YAKE

Msanii kutoka Nigeria Burna Boy ameendelea kurushiana maneno na mashabiki wa Wizkid, kupitia mtandao wa Twitter ameshambuliana nao tena hadi kutishia kumpiga Wizkid. Burna Boy alijikuta akiingia kwenye vita hiyo ya maneno baada ya mashabiki wa Wizkid kumvamia kwenye tweet yake ambayo aliweka mafanikio ya Album zake. Baada ya mashabulizi ya maneno kutoka kwa Wizkid FC, Burna Boy alikuja na kumwambia shabiki mmoja “Kama Wizkid asingekuwa rafiki yangu, basi kiukweli ningempiga ngumi ya uso papo hapo ili mashabiki zake wa Twitter wafahamu kwamba Mimi sio Davido. Lakini namshkuru Mungu ninafahamu na nimepevuka sana kufahamu (Wizkid) sio wewe.” aliandika Burna Boy kwenye tweet ambayo tayari imefutwa.

Read More
 BURNA BOY AWATOLEA UVUVI MASHABIKI WA WIZKID KWA KUMZUSHIA TAARIFA ZA UONGO

BURNA BOY AWATOLEA UVUVI MASHABIKI WA WIZKID KWA KUMZUSHIA TAARIFA ZA UONGO

Kumeibuka vita kati ya Burna Boy na mashabiki wa WizKid (Wizkid FC) kwenye mtandao wa Twitter. Burna Boy amewatupia vijembe kwamba wamekuwa wakimzushia vitu vya kijinga na kumtengenezea stori ambazo hazina ukweli wowote, na hii yote ni kutokana na kukosa elimu. “Niliwahi kusema kitu kama hichi kipindi cha nyuma lakini wafuasi wadanganyifu wa Wizkid (Wizkid FC) walisema nadanganya. Labda kama history ilikuwa inafundishwa kwenye shule zenu. Wizkid anapaswa kuwa na watu nadhifu hapa Twitter badala ya wajinga kama hawa.” aliandika Burna Boy na kuweka picha ya shabiki mmoja wa Wizkid. Shabiki mmoja alimuuliza kama zile insta stories zilizosambaa toka kwa Offset na ile iliyoonekana imetoka kwa Stefflon Don, zina ukweli? Burna Boy alijibu hapana, bali zilitengenezwa na mashabiki wapuuzi wa Wizkid FC. Burna alikuwa akiunga mkono kitu kilichosemwa na Professor aitwaye Wole Soyinka juu ya kuondolewa somo la Historia ya Nigeria kwenye mitaala ya elimu.

Read More
 WIZKID AWEKA REKODI APPLE MUSIC

WIZKID AWEKA REKODI APPLE MUSIC

Mwanamuziki nyota kutoka Nigeria Wizkid ameendelea kuweka rekodi haswa upande wa namba kwenye digital platforms mbalimbali. Taarifa njema kwa mashabiki wa staa huyo ni kwamba ameweza kuwa mwanamuziki wa kwanza Africa kupata zaidi ya streams billion 1 katika mtandao wa Apple Music. Wizkid pia amefikisha watazamaji millioni 1.3 YouTube , streams millioni 1.16 katika mtandao wa Spotify , jumla ya streams million 349 (total streams) Audiomack, streams 183 million Pandora na streams million 126 Boomplay.

Read More
 WIZKID ATHIBITISHA KUKAMILIKA KWA ALBUM YAKE MPYA

WIZKID ATHIBITISHA KUKAMILIKA KWA ALBUM YAKE MPYA

Staa wa muziki kutoka Nigeria Wizkid amethibitisha rasmi kukamilisha album yake mpya aliyoipa jina “More Love, Less Ego”. Kupitia Insta story yake  kwenye mtandao wa instagram wizkid amesema album hiyo  itatoka hivi karibuni. Hata hivyo Wizkid bado hajaweka wazi tarehe rasmi ya kuachia album hiyo mpya lakini ametoa shukrani kwa wote waliohusika katika uandaaji wake. Album hii mpya itaifuata “Made In Lagos” ambayo ilitoka Oktoba 30, mwaka 2020.

Read More