WIZKID MBIONI KUACHIA ALBUM MPYA
Album ijayo ya Wizkid itakuwa ya moto sana. Amethibitishia meneja wa zamani wa Chris Brown, Mike G kupitia ukurasa wake wa Twitter kwenye picha ambayo amepozi na mkali huyo kutoka nchini Nigeria. Mwezi Oktoba mwaka wa 2021 wakati akiwa kwenye ziara yake ya muziki ‘Made In Lagos’ Wizkid alitangaza kuwa Album yake ya Tano itaitwa “More Love, Less Ego” na itatoka mapema mwaka huu. Mike G kwa sasa anafanya kazi na mastaa wa dunia akiwemo Wizkid, Burna Boy, Young Thug na The Kid Laroi.
Read More