Entertainment

Toxic Lyrikali Amwaibisha Wakuu Music kwa Kuanika DM zake Akilizimisha Bifu

Toxic Lyrikali Amwaibisha Wakuu Music kwa Kuanika DM zake Akilizimisha Bifu

Rapa kutoka Kenya, Toxic Lyrikali, amezua gumzo kubwa mitandaoni baada ya kuanika jumbe za faragha za WhatsApp alizodai kutumiwa na Wakuu Music, akimshinikiza kuingia kwenye bifu naye kwa lengo la kuvuta umakini wa mashabiki.

Kupitia mitandao yake ya kijamii, Toxic ameshare screenshots za mawasiliano hayo zikimuonyesha Wakuu Music akimkabili kuhusu madai kuwa alikuwa amemdiss kwenye nyimbo zake. Hata hivyo, Toxic amekanusha madai hayo na kudai kuwa kinachoendelea ni juhudi za kulazimisha bifu ya kutengeneza headlines.

Hitmaker huyo wa Back Bencher, ameonekana kushangazwa na kitendo hicho, akisema kuwa ni jambo la kushangaza kuona mtu mzima bado anamtext akilazimisha ugomvi wa kisanii ili apate kuzungumziwa na mashabiki.

Kwa mujibu wa jumbe alizochapisha, Wakuu Music anaonekana kukerwa na madai kwamba amedharauliwa katika baadhi ya mistari ya ngoma za Toxic, jambo ambalo rapa huyo amekanusha na kudai kuwa hana mpango wa kuingia kwenye bifu la bandia kwa ajili ya hype.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *