Mdau wa burudani asiyeishiwa na matukio kila leo, Mwijaku, amezua gumzo mtandaoni baada ya kudai kuwa Bilionea Chief God Love amembebesha ujauzito msanii wake, Pipi Jojo.
Kwa mujibu wa Mwijaku, Pipi Jojo aliwahi kupata ujauzito wa awali ambao aliupoteza kupitia tukio la kuharibika kwa mimba (miscarriage). Hata hivyo, anadai kwa sasa msanii huyo ana ujauzito mwingine, na anasisitiza kuwa mimba hiyo ni ya Chief Godlove.
Mwijaku amesema hali hiyo ndiyo sababu kubwa inayomfanya Pipi Jojo asionekane sana mitandaoni na kwenye shughuli za kawaida za kazi siku za hivi karibuni.
Mwijaku ameenda mbali zaidi kwa kumtolea changamoto Chief Godlove, akimtaka ajitokeze hadharani na kumposti Pipi Jojo kama uthibitisho iwapo madai hayo ni ya uongo. Mwijaku ameonyesha kujiamini na kusisitiza kuwa anachokizungumza anakifahamu vizuri