
CEO wa Chama cha Content Creators nchini Kenya, Director Trevor amejitokeza na kumkingia kifua Diana B baada ya kupata ukosoaji mkali kutokana na wimbo wake mpya Bibi ya Tajiri ambao una zaidi ya views laki tano youtube ndani ya siku tatu.
Hii ni baada ya baadhi ya mashabiki na wakosoaji wa muziki kudai kuwa Diana hana kipaji cha uimbaji na uandishi wa muziki.
Akizungumza, Trevor amewataka Wakenya kumuunga mkono Diana badala ya kumbeza, akisisitiza kuwa kila msanii anastahili nafasi ya kujaribu na kukuza sanaa yake. Aidha, amewataka wasanii wa Kenya kushirikiana naye ili kuendeleza muziki wa ndani badala ya kumpuuza.
Trevor, hata hivyo, amesisitiza kuwa huu ni mwanzo wa safari ya Diana katika muziki na kwamba anastahili nafasi ya kuthibitisha kipaji chake.
Ukosoaji huo ulianza baada ya mashabiki kudai kuwa Bibi ya Tajiri ilikuwa sampled kutoka wimbo maarufu wa marehemu E-Sir, Sare Sare. Haikuishia hapo, baadhi walimlaumu Diana kwa kuchana picha za marapa wakubwa nchini kama Khaligraph Jones na Nyashinski kwenye video yake, wakisema kitendo hicho ni kukosea heshima muziki wa hip hop.