
Siku ya Valentine’s Day imeenda vibaya kwa rapa Kanye West na mchumba wake Julia Fox. Wawili hao wameripotiwa kuachana rasmi baada ya miezi miwili ya kuwa penzini.
Chanzo cha karibu kimeuambia mtandao wa TMZ kwamba YE na Fox wamebaki tu kuwa marafiki na washirika kwenye masuala mengine.
Kuisindikiza siku ya Valentine’s, Kanye West amemtumia Kim Kardashian maua ya kutosha kwenye gari lililofika hadi nyumbani kwake.
Rapa kanye west Ni kama bado anatamani kurudiana na Baby mama wake kim kardashian Kwa sababu anazidi kuja na matukio mbalimbali kila kukicha.