
Msanii wa Bongofleva Vanessa Mdee ni kama amenogewa na watoto, baada ya kumpata mtoto wake wa kwanza (Seven Adeoluwa Akinosho) na Rotimi mwezi Septemba mwaka huu.
Vee Money leo kupitia ukurasa wake wa Instagram,ametangaza matamanio yake ya kuongeza mtoto mwingine.
Vanessa ameweka video ya Rotimi akimbebeleza mtoto wao huyo wa Kiume na kisha kuacha caption ambayo mwisho alimalizia kwa kusema “Baby number two loading” akimaanisha mtoto wa pili yupo njiani.
Itakumbukwa kwenye moja ya mahojiano aliyowahi kufanya, Vee alinukuliwa akisema anatamani kuwa na watoto wawili.