Entertainment

Vera Sidika Amuomboleza Raila Odinga Katika Siku ya Mashujaa

Vera Sidika Amuomboleza Raila Odinga Katika Siku ya Mashujaa

Socialite wa Kenya, Vera Sidika, ameonyesha huzuni yake kubwa kufuatia kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya, Raila Amolo Odinga, akimkumbuka kama shujaa wa kweli wa taifa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Vera amechapisha ujumbe wenye hisia kali akieleza kuwa maadhimisho ya Mashujaa Day mwaka huu yamekuwa tofauti kwani yanakuja siku tano tu baada ya taifa kumpoteza kiongozi huyo mashuhuri.

Mama huyo wa watoto wawili, amesema kuwa bado haamini kwamba Raila hayupo tena duniani na kueleza kuwa mwaka huu kumbukumbu ya kuzaliwa kwa binti yake Asia imegubikwa na huzuni kubwa. Kwa mujibu wake, Raila atabaki kuwa shujaa wa kweli ambaye aligusa maisha ya Wakenya wengi.

Vera ameongeza kuwa mchango wa Raila katika historia ya Kenya na mapambano ya demokrasia hautasahaulika kamwe. Kifo cha kiongozi huyo kimeendelea kugusa watu kutoka nyanja mbalimbali, huku mashabiki, viongozi, na wasanii wakiendelea kumuenzi kama shujaa wa kizazi chake aliyejitolea kwa haki, umoja, na maendeleo ya taifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *