Entertainment

Vera Sidika awatolea uvivu wanaokosoa nywele za binti yake Asia Brown

Vera Sidika awatolea uvivu wanaokosoa nywele za binti yake Asia Brown

Soshalaiti maarufu mtandaoni kutoka nchini Kenya Vera Sidika ameshindwa kuwavumilia wanaokashifu mtindo wa nywele ya binti yake mchanga Asia Brown ambayo alikuwa amesukwa  kwenye kumbukizi ya siku ya kuzaliwa kwake.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Vera amesema watu wanaomunyoshea kidole cha lawama kuwa anamtesa binti yake kwa kumwekea nywele nzito kichwani ni malimbukeni kwani nywele zilizotumika kumsuka sio nzito kama inavyodaiwa mtandaoni.

Aidha mrembo huyo ambaye amegeukia muziki amesema hawezi kumudhuru mwanae na kitu asichokijua, hivyo watu waache kumsema vibaya kama mama asiyejali maslahi ya binti yake.

Kauli ya Vera Sidika imekuja baada ya walimwengu mtandaoni kumkashifu kwa hatua ya kutumia nywele aina braids kumsuka binti yake kitendo ambacho wengi walihoji kuwa mrembo analimdhulumu mtoto huyo mchanga kwa kumbebesha nywele nzito kichwani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *