Socialite wa Kenya, Vera Sidika, amethibitisha kwamba amefanyiwa upasuaji wa mdomo (lip procedure) wiki chache tu baada ya kupitia upasuaji wa kuinua maziwa (breast lift).
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Vera amesema kuwa upasuaji huo ni sehemu ya safari yake ya kujiboresha na kurejesha muonekano anaoupenda. Ameongeza kuwa yuko kwenye hatua ya kupona, na matokeo ya mwisho yatakuwa bora zaidi katika siku chache zijazo.
Vera pia amewaonya mashabiki wake wasishangae wakimuona na mdomo uliofura wakati wa club appearances atakazozifanya wiki hii, akisema ni hali ya kawaida baada ya upasuaji huo.
Tangazo hilo limezua gumzo mitandaoni, huku baadhi ya mashabiki wakimpongeza kwa uaminifu wake wa kushiriki safari ya urembo hadharani, na wengine wakijadili jinsi mitindo ya vipodozi na upasuaji wa kuboresha miili inavyozidi kupata umaarufu miongoni mwa watu mashuhuri nchini.