Gossip

Victoria Afichua Changamoto za Kuchumbiana na Kijana Mdogo

Victoria Afichua Changamoto za Kuchumbiana na Kijana Mdogo

Mwanamuziki Victoria Kimani amefichua kuwa aliwahi kujaribu kuwa kwenye mahusiano na mwanaume aliye mdogo kwake kiumri, lakini uhusiano huo haukufanikiwa kutokana na tofauti za mitazamo na mienendo ya maisha.

Akiwa kwenye mahojiano na mtangazaji Betty Kyallo, Victoria ameeleza kuwa uzoefu huo ulimsaidia kujitambua zaidi na kuelewa kile anachokipa kipaumbele kwenye uhusiano.

Katika mazungumzo hayo, Betty Kyallo alimchangamsha kwa utani kwa kumwambia kwamba anaweza kumpa mwongozo wa jinsi ya kumudu mahusiano na mwanaume mdogo.

Kauli hiyo ilisababisha kicheko studioni na kuibua mijadala mitandaoni, huku mashabiki wakisubiri kuona kama Victoria ataamua kujaribu tena bahati yake katika kudate kijana mdogo, safari hii akiwa na msaada kutoka kwa Betty ambaye yupo kwenye mahusiano ya kimapenzi na kijana wa Gen Z.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *