Entertainment

Victoria Kimani Abadilika Kimtindo, Asema Atafunguka Zaidi Kwenye Documentary

Victoria Kimani Abadilika Kimtindo, Asema Atafunguka Zaidi Kwenye Documentary

Msanii nyota kutoka Kenya, Victoria Kimani, amewasha moto mitandaoni baada ya kufichua muonekano mpya wa kipara, hatua aliyoiita mwanzo wa sura mpya katika maisha yake.

Kupitia mtandao wa Instagram, alichapisha picha mbalimbali zenye ujumbe wa kina, akieleza safari ya kujitambua, kuamka kiroho, na kuenzi urithi wa Kiafrika.

Katika mfululizo wa picha hizo, alionesha taswira ya simba akifuatisha na ujumbe wa kutambua nguvu ya kipekee ya mtu binafsi, mawingu yaliyochanwa na mwanga kama ishara ya kujifunua katika hali halisi, na picha za viongozi wa Kiafrika kama Mandela, Nyerere, Kenyatta na Kofi Annan, kuenzi uongozi na roho ya bara la Afrika.

Aidha, alidokeza kuwa maudhui hayo yatakuwa sehemu ya filamu anayotarajia kuzungumzia hivi karibuni, huku akimalizia na picha iliyoandikwa “A course by Victoria Kimani”, kuashiria ujio wa mradi maalum kutoka kwake.

Mashabiki wake wameonesha hamasa kubwa, wakisubiri kwa hamu kile kinachofuata kutoka kwa msanii huyo anayejulikana kwa ubunifu wa hali ya juu na maudhui yenye maana ya kina.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *