Gossip

Video Mpya Yazima Uvumi: Cardi B na Stefon Diggs Wapo Bado Kwenye Mahaba

Video Mpya Yazima Uvumi: Cardi B na Stefon Diggs Wapo Bado Kwenye Mahaba

Tetesi kuwa uhusiano kati ya rapa maarufu Cardi B na mcheza mpira wa Marekani Stefon Diggs umeenea mitandaoni, lakini taarifa mpya zinaonyesha kuwa penzi lao bado lipo imara.

Uvumi wa kuachana kwao ulianza baada ya mashabiki kubaini kuwa Cardi B alikuwa amefuta picha zote za Stefon Diggs kwenye akaunti yake ya Instagram, jambo lililoibua maswali mengi kuhusu mustakabali wa uhusiano wao.

Hata hivyo, Cardi B alionekana kupuuzilia mbali uvumi huo kwa kuchapisha video kupitia ukurasa wake wa X (zamani Twitter), akionekana akiwa gym na Diggs wakifanya mazoezi pamoja. Video hiyo imechukuliwa kama jibu kwa waliodhani kuwa wawili hao tayari wameachana.

Chanzo cha karibu na wawili hao kimeripotiwa kuiambia TMZ kwamba wapenzi hao bado wako kwenye mahusiano ya kimapenzi na wanaendelea vyema, tofauti na taarifa zinazozunguka mtandaoni.