
Hatimaye video za staa wa muziki nchini Otile Brown zimerudi youtube baada ya kuondolewa kwa siku kadhaa.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram staa huyo amewajuza mashabiki zake kuwa video hizo zimerudi rasmi baada ya kuondolewa youtube huku akiwashukuru mashabiki wake kwa kumuvumilia yeye pamoja na timu yake wakati walipokuwa wanafuatilia suala la kurejesha nyimbo zake kwenye mtandao huo.
Such kinda love, Dusuma, Chaguo la moyo wangu, Regina,Aaiyana ni kati ya video za nyimbo za Otile Brown ambazo ziliondolewa kwenye akaunti yake ya youtube.
Kurejeshwa kwa nyimbo hizo kumekuja siku chache baada ya staa huyo kutoa taarifa rasmi, akielezea utata unaozingira suala la kufutwa kwa nyimbo zake.
Hata hivyo otile brown hajaweka wazi sababu ya kuondolewa kwa video hizo