Kundi maarufu la muziki Vijana Baru Baru limekiri kuwa licha ya mafanikio makubwa waliyopata katika tasnia ya muziki, bado wanahisi hofu na mashaka ya kusherehekea matunda ya juhudi zao.
Akizungumza katika mahojiano na mtangazaji Alex Mwakideu, kundi hilo limefichua kuwa mara nyingi wanajizuia kusherehekea mafanikio yao kwa hofu ya kukosolewa na umma. Wamesema hata kununua gari jipya walihisi ni jambo la kuogopesha kushirikisha hadharani, wakihofia mtazamo wa watu na uwezekano wa kupoteza walichopata.
Licha ya nyimbo zao kupata mafanikio makubwa na kuvutia mashabiki wengi, Vijana Baru Baru wamesema mara chache sana wanasherehekea hadharani mafanikio hayo.
Kwao, hofu ya kupoteza kila kitu imeendelea kuwa kivuli kinachowafuata, na kuwafanya waishi kwa unyenyekevu mkubwa.