Nguli wa muziki kutoka Uganda, Jose Chameleone, ameibua gumzo kubwa baada ya kuonesha gari lake jipya aina ya Tesla Cybertruck. Hatua hii inamweka kwenye ramani ya mastaa wakubwa barani Afrika wanaomiliki moja ya magari ya kifahari na ya kisasa zaidi duniani.
Kupitia video inayosambaa mtandaoni Chameleone ameonekana akiwa anaendesha Tesla Cybertruck yake mpya ambapo mashabiki wamempongeza kwa mafanikio hayo makubwa.
Hata hivyo, kinachomtofautisha Chameleone ni kuwa msanii wa kwanza kutoka Afrika Mashariki kumiliki gari hili, jambo linaloongeza hadhi yake na kuonesha upeo mpya wa mafanikio katika tasnia ya muziki.
Chameleone anajiunga na orodha ya majina makubwa katika muziki wa Afrika kama Timaya, Davido, Omah Lay, na Asake, ambao tayari wanamiliki Tesla Cybertruck.