Entertainment

VJ Patelo Amshambulia Toxic Lyrikali kwa Kuishi Maisha ya Feki

VJ Patelo Amshambulia Toxic Lyrikali kwa Kuishi Maisha ya Feki

Msanii wa Arbantone VJ Patelo ameibua upya mzozo na msanii wa hip-hop Toxic Lyrikali, akimtuhumu kuishi maisha bandia na kukosa ubunifu katika muziki wake.

Kupitia ujumbe aliouchapisha kwenye mitandao ya kijamii, Patelo amedai kuwa Lyrikali hudanganya katika mashairi ya muziki kuhusu utajiri na mali anazomiliki, ikiwemo madai ya kuwa na gari la kifahari aina ya Mercedes-Benz S-Class. Amesema kuwa msanii huyo anaishi maisha ya kuigiza na kwamba madai yake kuhusu magari na pesa ni ya kutafuta umaarufu tu.

Patelo pia ameongeza kuwa nyimbo nyingi za Lyrikali si za asili, akidai kwamba amekuwa akiiga nyimbo za wasanii wa Jamaica na kuzitafsiri kwa Sheng ili kuwavutia mashabiki wa muziki nchini Kenya. Amesema hakuna ubunifu wa kweli katika kazi zake, bali ni nakala za nyimbo za nje zilizotiwa ladha ya mitaani.

Kauli za Patelo zimezua gumzo mitandaoni, huku mashabiki wakigawanyika kati ya wanaomuunga mkono na wale wanaomtetea Toxic Lyrikali. Hadi sasa, msanii huyo hajatoa majibu rasmi kuhusu tuhuma hizo, ingawa hii si mara ya kwanza anakosolewa kuhusu uhalisia wa nyimbo zake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *