Entertainment

Vybz Kartel avunja ukimya baada ya kufutwa kwa onyesho lake nchini Trinidad

Vybz Kartel avunja ukimya baada ya kufutwa kwa onyesho lake nchini Trinidad

Msanii nguli wa muziki wa dancehall kutoka Jamaica, Vybz Kartel, amevunja ukimya kufuatia kufutwa kwa onyesho lake lililokuwa limepangwa kufanyika leo katika One Caribbean Festival nchini Trinidad.

Kupitia taarifa kwa vyombo vya habari, msanii huyo mashuhuri wa dancehall alieleza kuwa licha ya kutoa ushauri mara kadhaa kwa waandaaji wa tamasha hilo kuhusu hatua muhimu zinazopaswa kuchukuliwa, matatizo hayo hayakutatuliwa kwa wakati. Kartel alifichua kuwa alitoa onyo mapema ili kuhakikisha kuwa kila kitu kinaenda sawa, lakini ushauri wake haukufanyiwa kazi ipasavyo.

Msanii huyo pia aliwaomba radhi watu wa Trinidad na mashabiki wake waliokuwa wakisubiri kwa hamu kumpa sapoti jukwaani.

“Nimesikitishwa sana na jinsi mambo yalivyokwenda. Mashabiki wangu walistahili burudani, na ninawaahidi kuwa nitafanya kila niwezalo kuhakikisha kuwa hali kama hii haitajirudia,” alisema Vybz Kartel.

Mashabiki wengi wameeleza masikitiko yao kwenye mitandao ya kijamii huku wakimtaka msanii huyo kupanga upya onyesho hilo mara tu matatizo yaliyopo yatakapotatuliwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *