Entertainment

Vybz Kartel na Mavado Waungana Tena Baada ya Miaka 17 ya Bifu la Gaza vs Gully

Vybz Kartel na Mavado Waungana Tena Baada ya Miaka 17 ya Bifu la Gaza vs Gully

Wasanii wawili maarufu wa dancehall kutoka Jamaica, Vybz Kartel na Mavado, wamezua gumzo kubwa baada ya kuungana tena rasmi kwa mara ya kwanza tangu bifu lao kali la mwaka 2008 maarufu kama “Gaza vs Gully”. Wawili hao, waliowahi kugawanya mashabiki wa muziki wa dancehall kwa kambi pinzani za Gaza (Kartel) na Gully (Mavado), sasa wameamua kuzikana tofauti zao na kushirikiana kwenye wimbo mpya unaotarajiwa kutikisa ulimwengu wa muziki.

Kwa mujibu wa taarifa zilizothibitishwa, Vybz Kartel na Mavado wanashirikiana na DJ Khaled pamoja na gwiji mwingine wa dancehall, Bounty Killer, kwenye mradi huu mpya wa muziki. Ushirikiano huu si tu kwamba ni wa kihistoria, bali pia ni ujumbe mzito wa mshikamano na mabadiliko katika tasnia ya muziki wa Caribbean.

Mashabiki duniani kote wamesema hawakuamini macho yao walipoona picha na video za wasanii hao wakirekodi pamoja. Wengi wamefurahia hatua hiyo wakisema imeleta matumaini mapya katika mwelekeo wa muziki wa dancehall.

Wimbo huo mpya unatarajiwa kutolewa ndani ya wiki chache zijazo na tayari unahesabiwa kama moja ya collabo kubwa zaidi katika historia ya dancehall. Mashabiki wanasubiri kwa hamu kusikia ladha ya muziki huo ambao unawakutanisha tena magwiji waliowahi kuwa mahasimu wakubwa.