
Lejendari wa muziki nchini Nameless amethibitisha kuwa mke wake Wahu amejifungua mtoto wa kike.
Nameless ameeleza furaha yake kupitia mitandao yake ya kijamii kwa Wahu kujifungua salama, akimshukuru Mungu pamoja na mashabiki zake ambao wamekuwa mstari wa mbele kuwaombea dua kwa kusema kuwa mke yupo tayari kwa majukumu ya kumlea mtoto wao
Aidha amesema mtoto huyo wa kike ambaye amepewa jina la kumuenzi dada yake mkubwa kulingana na tamaduni za jamii ya Kikuyu, anaitwa Shiru.
Ni hatua ambayo imepokelewa kwa furaha na mastaa wenzake kutoka Kenya ambao walitupia comment zao kwenye posti yake wakimtakia heri pamoja na mke wake Wahu.
Huyu anakuwa mtoto wa tatu kwa Nameless na Wahu Kagwi ambao wametimiza miaka 17 wakiwa mume na mke ikizingatiwa tayari katika ndoa yao wamebahatika kupata watoto wawili, wote wakiwa wakike.