
Wanamuziki David Mathenge maarufu kama Nameless na Wahu Kagwi wametimiza miaka 17 ya ndoa na miaka 25 tangu wayaanze mahusiano yao.
Wawili hao ambao walianza mahusiano yao mwaka 1997 walifanikiwa kufunga ndoa mwaka 2005 na katika ndoa yao wamebahatika kupata watoto wawili, wote wakiwa wakike.
Leo, Septemba 10 ni anniversary yao, ambapo wametimiza miaka 12 wakiwa mke na mume. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Nameless ambaye ndiye mume wa Wahu ameandika haya..
“Happy Anniversary Babe! 17 years today since we said ” I DO!” and 25 years since our first date! And you still the ONE ! Just alittle heavier !! Thank you for taking this journey of life with me! ”
Ndoa ya wanamuziki hao imedumu muda mrefu kinyume na matarajio ya wengi kutokana na jinsi watu maarufu wamekuwa wakiacha ndoa zao ulimwenguni kote.
Utakumbuka kwa sasa Nameless na Wahu wanatarajia kupata mtoto wao wa tatu hivi karibuni.