
Bosi wa Gagamel, Msanii Bebe Cool ana imani kuwa wasanii wa Uganda wataendelea kung’aa kimataifa kupitia muziki wao.
Kwenye mahojiano yake hivi karibuni, Bebe Cool amebainisha kuwa kuteuliwa kwa Eddy Kenzo kwenye tuzo za Grammy 2023 itawafungulia wasanii wengi nchini humo milango ya kushiriki tuzo kubwa duniani.
Ikumbukwe kipindi cha nyuma Bebe Cool alikuwa kwenye ugomvi (bifu) na Eddy Kenzo mara baada ya hitmaker huyo wa “Nsimbudde” kukimbia na msanii wake Rema Namakula ambaye alikuwa chini ya Gagamel Entertainment. Lakini wawili hao walikuja wakaweka kando tofauti zao kwa manufaa ya tasnia ya muziki nchini Uganda.