
Wasanii wa muziki kutokea nchini Nigeria, Burna Boy na Tems wametajwa kuwania vipengele viwili kila mmoja katika Tuzo za Grammy 2022.
Burna Boy ametajwa kwenye vipengele viwili, “Best Global Music Performance” kwa ngoma yake ya “Last Last” na kingine ni “Best Global Music Album” – Love Damini.
Naye Tems ametajwa kwenye vipengele viwili kama “Best Melodic Rap Performance” kupitia ngoma aliyoshirikishwa na future Ft Drake – Wait For You na pia “Best Rap Song” – Wait For You.