Entertainment

WEEZDOM ALAMBA SHAVU LA KUWA BALOZI WA KAMPUNI YA UWEKEZAJI YA LIMAVEST

WEEZDOM ALAMBA SHAVU LA KUWA BALOZI WA KAMPUNI YA UWEKEZAJI YA LIMAVEST

Msanii wa muziki nchini Weezdom amelamba dili nono la kuwa balozi wa kampuni ya uwekezaji ya Limavest.

Weezdom ametengaza habari hiyo njema kwa mashabiki zake kupitia ukurasa wake wa instagram huku akieleza kuwa ana furaha kujiunga na familia ya LimaVest

“Najivunia Kukutangazia Kuwa Mimi ndiye Balozi Mpya wa limavest Na tuna Bidhaa mpya yenye bei nafuu Ulizowahi Kufikiria.. Kwa shillingi laki 350 tu…unaweza kushtua kijiji chako kwa kuwapa kitu cha dhamani ambacho kitabadilisha maisha yao na kukutengenezea pesa” aliandika Weezdom kupitia Instagram yake.

Weezdom sasa atatakiwa kutangaza bidhaa za  Limavest kwa mashabiki zake kupitia mitandao ya kijamii kwa lengo la kuongezea kampuni hiyo wateja.

Limavest ni kampuni ya uwekezaji ambayo huwapa wateja wake fursa sio tu ya kumiliki mali, lakini pia kutumia mali hiyo kuchuma riziki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *