Tech news

WhatsApp Yaja na Maboresho Mapya ya Kusafisha Storage Kwenye iOS

WhatsApp Yaja na Maboresho Mapya ya Kusafisha Storage Kwenye iOS

WhatsApp inaendelea kuboresha uzoefu wa watumiaji wake, na safari hii inaleta mabadiliko mapya kwenye sehemu ya kusafisha Storage kwa watumiaji wa iOS. Maboresho haya yanalenga kuwasaidia watumiaji kudhibiti kwa urahisi nafasi ya hifadhi (storage) kwenye simu zao.

Kwa mujibu wa mabadiliko mapya, WhatsApp itabadilisha muonekano na utendaji wa sehemu ya kusafisha Storage na kuweka njia rahisi zaidi ya kupunguza ukubwa wa video, chats na documents ambazo huchukua nafasi kubwa ya hifadhi. Watumiaji sasa wataweza kuona kwa uwazi ni aina gani ya media inayotumia storage nyingi zaidi.

Mfumo huu mpya utaruhusu kuchagua aina maalum za media kama picha au video, na utaonyesha kwa kina kiasi cha hifadhi kinachotumiwa na kila aina. Zaidi ya hapo, mtumiaji ataweza kufuta media kwa pamoja kulingana na aina au format ya files, badala ya kufuta moja moja kama ilivyokuwa awali.

Mabadiliko haya yanatarajiwa kurahisisha usimamizi wa storage, hasa kwa watumiaji wanaopokea au kutuma media nyingi kila siku. Hatua hii inaonyesha dhamira ya WhatsApp kuendelea kuboresha programu yake kulingana na mahitaji ya watumiaji wa iOS.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *