Sports news

Uganda Kukutana na Nigeria Leo Jioni kwenye Pambano la Kundi C AFCON

Uganda Kukutana na Nigeria Leo Jioni kwenye Pambano la Kundi C AFCON

Uganda na Nigeria zinakutana tena leo jioni katika mchuano wa Kundi C wa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) kwenye Uwanja wa Complex Sportif de Fès.

Hii ni mara ya pili kwa timu hizo kukutana katika hatua ya fainali za AFCON, baada ya mechi yao ya kihistoria mwaka 1978 ambapo Uganda iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Nigeria katika nusu fainali.

Katika mchuano mwingine wa Kundi C, Tanzania itapambana na Tunisia kwenye Uwanja wa Prince Moulay Abdellah mjini Rabat. Nigeria inaongozakundi C kwa alama sita, tatu mbele ya Tunisia iliyo nafasi ya pili. Tanzania inashikilia nafasi ya tatu kwa alama moja, ikiwazidi Uganda kwa tofauti ya mabao.

Hii ni hatua muhimu kwa timu zote, kwani matokeo ya leo yanaweza kubadilisha kabisa taswira ya Kundi C na kuamua ni nani atakayeendelea katika hatua inayofuata.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *