Staa wa muziki kutoka nchini Kenya, Willy Paul, ameelezea masikitiko yake kuhusu jinsi mashabiki wa muziki wa Kenya wanavyomchukulia poa, akidai kuwa licha ya mafanikio yake makubwa kimataifa, bado hatambuliwi ipasavyo nyumbani.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, msanii huyo amesema kuwa yeye ndiye msanii pekee wa Kenya ambaye nyimbo zake zinachezwa zaidi kimataifa kuliko za wasanii wengine wengi, lakini mashabiki wa ndani wanapuuzia juhudi zake.
Willy Paul amesisitiza kuwa ukweli unabaki kuwa yeye ndiye msanii anayejulikana zaidi nje ya nchi na anaamini kuwa muda utakuja ambapo mashabiki wa nyumbani watatambua thamani ya kazi zake.
Kauli yake imekuja baada ya content creator wa mitandaoni Ruth K kumtaja kama msanii wa kimataifa anayepaswa kupewa heshima zaidi kutokana na ushawishi wake nje ya mipaka ya Kenya.