Gossip

Wivu wa Paula Wamchelewesha Marioo Kuachia Video Mpya

Wivu wa Paula Wamchelewesha Marioo Kuachia Video Mpya

Msanii wa Bongo Fleva, Marioo, amefunguka kuwa kuchelewa kwake kuachia video yake mpya kumetokana na wivu wa mpenzi wake, Paula Kajala, ambaye ni binti wa muigizaji maarufu Frida Kajala.

Kupitia Instagram, Marioo amesema alitarajia kutoa video hiyo jana kama alivyoahidi kwa mashabiki wake, lakini Paula alimzuia kutokana na baadhi ya vipande vilivyomo kwenye video hiyo ambavyo hakuridhika navyo.

Mkali huyo wa ngoma ya Dunia, ameeleza kuwa mpenzi wake alionyesha wivu mkubwa akisema kuna sehemu ambazo hazimpendezi, ingawa yeye binafsi hakuona tatizo lolote katika picha hizo.

Marioo ameongeza kuwa amewekeza fedha nyingi katika utayarishaji wa video hiyo, na kuchelewa kwake kumeathiri ratiba aliyokuwa amepanga kwa ajili ya mashabiki wake.

Hadi sasa, Marioo hajatangaza tarehe mpya ya kuachia video hiyo, lakini amesema anafanya jitihada za kutatua tofauti hizo ili mashabiki wake wapate kazi hiyo muda si mrefu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *