Msanii wa muziki kutoka Kenya, Akothee, amezua mjadala mitandaoni baada ya kutoa matamshi yenye utata kuhusu wanaume wa Kanisa la Waadventista (SDA).
Kupitia video aliyoiposti kwenye mitandao yake kijamii, amesema kuwa hawezi kamwe kuolewa na mwanaume kutoka kanisa hilo kwa kuwa wanaume wengi wa SDA ni wakali na wenye masharti mengi kuhusu maisha ya kila siku, jambo analoliona haliendani na mtindo wake wa maisha.
Mwanamama huyo ameongeza kuwa hawezi kuishi kwenye ndoa inayomnyima uhuru wa kufurahia maisha, akitaja mambo kama kunywa mvinyo na kula nyama kuwa sehemu ya starehe anazopenda.
Hata hivyo amesema kuwa licha ya yeye mwenyewe kuwa Mwaadventista, bado hawezi kumpendekeza mtu kuolewa na wanaume kutoka dhehebu hilo.