Gossip

Zari Hassan Atishia Kuwaanika Wanawake Wanaomtaka Mtoto Wake wa Kiume Kimapenzi

Zari Hassan Atishia Kuwaanika Wanawake Wanaomtaka Mtoto Wake wa Kiume Kimapenzi

Socialite maarufu mwenye asili ya Uganda, Zari Hassan, ameonyesha kuchoshwa na wanawake wanaoendelea kumuandikia mwanawe wa kiume jumbe za mahaba wakionyesha nia ya kumtaka kimapenzi.

Kupitia kauli yake mitandaoni, Zari amesema amekuwa akipokea DM nyingi kutoka kwa wanawake wanaojitokeza waziwazi kumtongoza mtoto wake, hali anayosema imevuka mipaka na kumkera.

Mwanamama huyo, ameweka wazi kuwa mwanawe tayari yuko kwenye mahusiano na binti wa kizungu, huku akiwataka wanawake hao kuacha tabia ya kumtumia jumbe za kumtamani kimapenzi (thirsty messages). Ameonya wakiendelea na tabia hiyo huenda akachukua maamuziki magumu ya kuwaanika mtandaoni.

Kauli ya Zari imezua mijadala mitandaoni, baadhi wakimuunga mkono kwa kulinda faragha ya mwanawe, huku wengine wakiona ni athari ya umaarufu unaoambatana na familia za mastaa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *